MAISHA YA MTAKATIFU NIKOLA WA TOLENTINO
Mama wa Mtakatifu huyu alikuwa mzee bila watoto na ndiyo maana alisikitika sana rohoni mwake.
Mwisho akaukimbilia msaada wa Mtakatifu Nikola (Tunayemkumbuka Desemba 6) ili amwombee kwa Mungu amjalie kupata mtoto.
Pamoja na Mume wake, walikwenda kuhiji katika Kanisa la Mtakatifu Nikola wa Mira huko Bari katika mpaka wa Italia na mwaka uliofuata wakazaa mtoto na kumwita jina lake Nikola.
Nikola alifuata mfano wa somo wake Mtakatifu. Alipokua alijiunga na Shirika la watawa wa Mtakatifu Augustino mjini Tolentino.
Akafuata mfano wa Watawa wengine akafanya bidii ya kujiendeleza katika fadhila zote.
Alipadrishwa akawa mhubiri hodari.
Alifariki mjini Tolentino mwaka 1305, akatangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1446. Inasemekana kwamba siku moja alipokuwa ameugua sana alipewa mkate akamwomba Bikira Maria kumpatia nafuu ya ugonjwa wake.
Nikola aliula mkate ule na mara akapona ndiyo maana kila mwaka katika sikukuu ya Mtakatifu Nikola wa Tolentino Mapadre wa Shirika la Mtakatifu Augustino hubariki mikate kwa kuwatuliza Wagonjwa wanaoomba na kutumaini msaada wa Bikira Maria na Mtakatifu Nikola.
MTAKATIFU NIKOLA, UTUOMBEE..

Post a Comment