Somo la Kwanza
Ufu
7:2-4,9-14
Mimi Yohane, niliona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-kondoo. Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina. Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa aliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Nao wametoka wapi? Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo
wa Katikati
Zab
24:1-6
Nchi
na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia
na wote wakaao ndani yake.
Maana
ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na
juu ya mito ya maji aliithibitisha.
(K)
Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Ni
nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni
nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu
aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua
nafsi yake kwa ubatili.
(K)
Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Atapokea
Baraka kwa Bwana,
Na
haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki
ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao
uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
(K)
Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Somo
la Pili
1Yoh
3:1-3
Tazameni,
ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo
tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini
twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama
alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo
mtakatifu.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Shangilio
Mt
11:28
Aleuya,
aleluya.
Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na
mizigo, nami nitawapumzisha, asema Bwana.
Aleluya.
Somo
la Injili
Mt
5:1-12
Yesu
alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake
walimjua; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
Heri
walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri
wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
Heri
wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Heri
wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Heri
wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Heri
wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Heri
wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Heri
wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri
ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa
ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni;
kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Neno la Bwana, Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment