Somo
la Kwanza
Ybs
35:12-14,16-19
Kwa kuwa Bwana ndiye mhukumu wala hakijali cheo cha mtu. Hatamkubali ye yote juu ya maskini, naye ataisikiliza sala yake aliyedhulumiwa. Hatayadharau kamwe malalamiko ya yatima, wala ya mjane amwelezapo habari zake. Malalamiko yakealiyeonewa yatapata kukubaliwa, na dua yake itafika hima mbinguni. Sala yake mnyenyekevu hupenya mawingu; wala haitatulia hata itakapowasili; wala haitaondoka hata Aliye juu atakapoiangalia, akaamua kwa adili, akatekeleza hukumu. Wala Bwana hatalegea, walahatakuwa mvumilivu kwa wanadamu.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo
wa Katikati
Zab
34:1-2, 16-18, 22
Nitamhimidi
Bwana kila wakati,
Sifa
zake zi kinywani mwangu daima.
Katika
Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu
wasikie wakafurahi.
(K)
Maskini huyu aliita Bwana akasikia
Uso
wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe
kumbukumbu lao duniani.
Walilia,
naye Bwana akasikia,
Akawaponya
na taabu zao zote.
(K)
Maskini huyu aliita Bwana akasikia
Bwana
yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na
waliopondeka roho huwaokoa.
Bwana
huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala
hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.
(K)
Maskini huyu aliita Bwana akasikia
Somo
la Pili
2 Tim
4:6-8, 16-18
Mimi
sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo
vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya
haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu,
bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. Katika jawabu langu la
kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba
wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia
nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie
Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bwana ataniokoa na kila
neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye
milele na milele. Amina.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Shangilio
Yn
8:12
Aleluya,
aleluya
Mimi
ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya
Somo
la Injili
Lk
18:9-14
Yesu
aliwaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau
wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa
pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu,
nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu,
wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa
zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala
hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema,
Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda
nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye
atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Neno a Bwana, Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment