Somo
la Kwanza
Rum
9:1-5
Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu, ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili; ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo
wa Katikati
Zab
147:12-15, 19-20
Msifu
Bwana, Ee Yerusalemu;
Msifu
Mungu wako, Ee Sayuni.
Maana
ameyakaza mapingo ya malango yako,
Amewabariki
wanao ndani yako.
(K)
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Ndiye
afanyaye Amani mipakani mwako,
Akushibishaye
kwa unono wa ngano.
Huipeleka
amri yake juu ya nchi,
Neno
lake lapiga mbio sana.
(K)
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Humhubiri
Yakobo neno lake,
Na
Israeli amri zake na hukumu zake.
Hakulitendea
taifa lolote mambo kama hayo,
Wala
hukumu zake hawakuzijua.
Aleluya.
(K)
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Shangilio
Zab
119:34
Aleluya,
aleluya,
Unifahamishe
nami nitaishika sheria yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
Somo
la Injili
Lk
14:1-6
Yesu
alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku
ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. Na tazama, mbele yake palikuwa na
mtu mwenye ugonjwa wa safura. Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na
Mafarisayo, Je! Ni halali kuponywa siku ya sabato, ama sivyo? Wao wakanyamaza.
Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake. Akawaambia, Ni nani miongoni
mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara
hiyo siku ya sabato? Nao hawakuweza kujibu maneno haya.
Neno la Bwana, Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment