Rum
8:26-30
Roho hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab
13:3-6
Ee
Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;
Uyatie
nuru macho yangu,
Nisije
nikalala usingizi wa mauti.
Adui
yangu asije akasema, Nimemshinda;
Watesi
wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
(K)
Nimezitumainia fadhili zano, Ee Bwana.
Nami
nimezitumainia fadhili zako;
Moyo
wangu na uufurahie wokovu wako.
Naam,
nimwimbie Bwana,
Kwa
kuwa amenitendea kwa ukarimu.
(K)
Nimezitumainia fadhili zano, Ee Bwana.
Somo
la Injili
Lk
13:22-30
Yesu
alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda
Yerusalemu. Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache?
Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana
nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. Wakati mwenye nyumba
atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha
mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui
mtokako; ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe
ulifundisha katika njia zetu. Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako;
ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Ndipo kutakapokuwa na
kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote
katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. Nao watakuja watu toka
mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani
katika ufalme wa Mungu. Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza,
na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
Neno la Bwana, Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment