Somo la Kwanza
Rum
8:12-17
Kama ni hivyo, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili; kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo
wa Katikati
Zab
68:1,3,5-6,19-20
Mungu
huondoka, adui zake wakatawanyika,
Nao
wamchukiao huukimbia uso wake.
Bali
wenye haki hufurahi,
Na
kuushangilia uso wa Mungu,
Naam,
hupiga kelele kwa furaha.
(K)
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa.
Baba
wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu
katika ko lake takatifu.
Mungu
huwakalisha wapweke nyumbani;
Huwatoa
wafungwa wakae hali ya kufanikiwa.
(K)
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa.
Na
ahimidiwe Bwana,
Siku
kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;
Mungu
ndiye wokovu wetu.
Mungu
kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;
Na
njia za kutoka mautini.
(K)
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa.
Shangilio
Ebr
4:12
Aleluya,
aleluya!
Neno
la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya
moyo.
Aleluya.
Somo
la Injili
Lk
13:10-17
Siku
ya sabato Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama,
palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane,
naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita,
akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu
yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.</p><p>Basi mkuu wa
sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu
akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe
katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akamjibu akasema,
Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, Je! Hamfungi ng’ombe wake au punda wake siku ya
sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa
Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa
afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote
walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu
yaliyotendwa na yeye.
Neno la Bwana, Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment