MAISHA YA MTAKATIFU LUKA, MWINJILI.

Alikuwa Mgiriki aliyezaliwa katika ukoo wa wapagani akaongoka na kushika dini ya Kikristo.

Mtume Paulo amemtaja kama Luka, daktari wetu mpenzi(Kol. 4:14).

Kisha kuulizia habari za wale walioandamana na Bwana wetu alipokuwa hapa duniani Luka akaandika Injii yake kwa mvuvio wa Roho Mtakatifu. 

Wakiwa wainjili Marko na Yohane, Luka na Matayo wameandika habari za utoto wa Bwana Yesu lakini kila mmoja wao ameiandika habari hiyo kwa namna yake. 

Hivyo ni Luka tu anayetusimulia habari ya kuzaliwa Yohani Mbatizaji kutokea kwa Malaika Gabrieli na kutolewa Yesu hekaluni. 

Baadaye Luka akaandika pia kitabu cha Matendo ya Mitume kinachoeleza kuhusu miaka ya kwanza ya Kanisa.

Mwandishi fulani wa karne ya pili ameandika kwamba Luka hakupata kuoa kamwe na pia kwamba alifia Ugiriki mwenye umri wa miaka themanini na minne. 

Wapo wengine wasemao kwamba aliteswa na kuuawa lakini hakuna uthibitisho wowote ule.

Katika picha Luka huoneshwa pamoja na ng'ombe, kwa maana mwanzoni mwa Injili yake ametoa habari ya Zakaria, kuhani wa Kiyahudi, ambaye kazi yake ilikuwa kumtolea Mungu sadaka za Wanyama.


MTAKATIFU LUKA MWINJILI, UTUOMBEE..

Post a Comment

Previous Post Next Post