Mt. Teresa wa Avila alizaliwa Hispania tarehe 28/3/1515 na Baba Alonso Sanchez na mama Beatrix. Walimlea katika maadili mema. Akiwa bado mdogo Teresa na kaka yake Rodrig walitoroka kwenda kuyatolea maisha yao kama mashahidi wakati wa madhulumu ya Moors. 

Teresa alijiunga na utawa akiwa na miaka 15, ambako aliishi kitakatifu akijikita katika sala na maonano ya Ekaristi takatifu. Alidhihirisha upole, unyenyekevu na nidhamu ya Maisha.

Mt. Teresa wa Avila aliandika na kufundisha mengi juu ya sala na akahimiza mabadiliko ya kweli katika maisha ya monasteri. Juu ya sala, Mt. Teresa anasema 
sala ni tendo la upendo, maneno hayahitajiki
hivyo anahimiza muunganiko wa ndani na wa kudumu. Tusali kwa moyo wa matumaini bila kukata tamaa.

Akiandika juu ya umisionari, Mt. Teresa wa Avila anasema 

naamini Mungu huwasaidia wale wanaotoka kwenda kutenda kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kamwe Mungu hawaangushi wale wote wanaomtumaini yeye peke yake.


Alifariki tarehe 4 Oktoba 1582 huko Salamanca. Alitajwa mwenyeheri tarehe 24/4/1614 na papa Paul V na tarehe 12/3/1622 alitangazwa kuwa mtakatifu na Papa Gregory XV. 

Kwa kazi yake njema ya kulifundisha kanisa na kutaka mabadiliko, Mt. Teresa wa Avila alipewa heshima ya kuwa Daktari /Mwalimu wa Kanisa.


Mt. Teresa wa Avila atujalie nasi tutumie vema karama na vipaji vyetu kwa ajili ya utukufu wa Mungu.


MTAKATIFU TERESA WA AVILA, UTUOMBEE..

Post a Comment

Previous Post Next Post