Karol Woljtyla ambaye ndiye Mtakatifu Yohane Paulo II alizaliwa 18 Mei 1920 huko Poland.
Alipokiwa na Miaka 20 alikuwa ameshapoteza wanafamilia wake wote yaani Baba, Mama na Dada yake.
Baada ya hapo, Alijiunga na Seminari kwa malezi ya Upadre na miaka yake ya malezi yaliathiriwa sana na vita kuu ya pili ya dunia.
Alipadrishwa Mwaka 1946 na alijiendeleza na masomo ya Teolojia huko Italia. Alichaguliwa kuwa Askofu mwaka 1964 na Kardinali mwaka 1967.
Mwaka 1978 alichaguliwa kuwa Papa wa 264 hadi mwaka 2005 alipofariki.
Yohane Paulo wa Pili ni Papa wa Tatu kukaa katika huduma hiyo kwa muda mrefu zaidi, baada ya Mtume Petro na Papa Pius wa X.
Wengi wanamhesabu kati ya watu walioathiri zaidi karne ya 20, hasa kwa sababu tangu mwanzo wa Upapa wake alipambana na Ukomunisti ulioitesa nchi yake ya asili kwa kiasi kikubwa.
Moja ya kazi zake kubwa akiwa Papa ni kufundisha Imani na Maadili na ndiye Papa aliyewahubiria watu wengi zaidi hadi leo.
Alifanya ziara 104 katika nchi 129 akiwa Papa, ikiwemo Tanzania mwaka 1990. Mwaka 1981 alinusurika kwenye jaribio la kupigwa risasi lililofanywa na Mehmet Ali Agca na baadaye alimsamehe.
Anakumbukwa pia kwa Kuleta mapatano na dini nyingine hasa Waislamu.
Alikuwa na Ibada kubwa kwa Mama Bikira Maria. Alifariki tarehe 02 Aprili 2005.
Baada ya utafiti na Ushujaa wa maandishi yake na miujiza kadhaa, alitangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014 na Papa Fransisko.
Sikukuu yake hufanywa tarehe 22 Oktoba, tarehe ambayo alifanya Misa yake ya kwanza kama Papa.
MTAKATIFU YOHANE PAULO II, UTUOMBEE..

Post a Comment