SIKU YA KWANZA
Baba Yosefu, ulimfundisha Yesu jinsi ya kusali,
kucheza na kufanya kazi, utusaidie kutambua kwamba tunaweza kupata elimu kwa
kusikiliza na kujifunza. Tukiwa na wewe ambaye unatusaidia na kutuongoza,
tunaomba, ee Mt. Yosefu, utuombee tuchague njia sahihi na tubaki kuwa waaminifu
katika mafundisho ya Yesu. Amina.
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA PILI
Mt. Yosefu, ulimwokoa na kumhudumia Neno wa Mungu, na
chakula cha uzima kilichoshuka kutoka mbinguni. Uwaangalie mapadri wa Kanisa,
ambao asili yao ni nyumba uliyoiongoza, na uwaombee ili nao pia, waweze
kuwahudumia kwa uvumilivu watu waliowekwa chini ya uangalizi wao. Tunaomba
mapadri wawafundishe kiaminifu waamini Neno la Mungu na kuumega mkate, wa uzima
kila siku, kwa ajili yao.Tunaomba wawaimarishe katika imani na matumaini,
wakiwafariji katika magumu na katika nyakati za kukukatisha tamaa. Pia umuombe
Yesu wetu awavishe taji kwa kazi zao na utumishi wao kwake hapa duniani kwa
kuwashirikisha uzima wa milele pamoja nawe Mbingguni milele na milele.
Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA TATU
Mt. Yosefu Mwenyeheri, sala zako zinaweza kufanya
mambo yasiyowezekana, yakawezekana. Tunakuomba uje kutusaidia katika shida na
magumu tuliyonayo sasa. Uweke kwenye ulinzi wako shida na mahangaiko yetu
tunayoyaleta kwako na utuombee, ili tuweze kupata msaada kadiri ya mapenzi ya
Mungu. Baba yetu mpendwa, tunakutegemea kabisa, na kwa imani, tunajikabidhi
kwako kama watoto wadogo waliyolala mikononi mwa baba zao. Isisemekane kamwe,
kwamba tumekuomba bila mafanikio. Yesu na Maria hawawezi kukukatalia chochote
unachowaomba. Kwa matumaini hayo, tunakuomba udhihirishe wema na Upendo wako
mkubwa kama ilivyo nafasi yako kwa mchumba wako, Bikira Maria, na Mwanao Yesu.
Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA NNE
Mpendwa Mt.
Yosefu, wewe ni msimamizi wa familia ya kanisa. Mungu alikuteua uwe kiongozi na
mlinzi wa Familia Takatifu ya Nazareti. Ulichagua kufanya kazi ya useremala,
amabayo iliwafanya baadhi ya watu waulizane juu ya Yesu wakisema; “Huyu amepata
wapi hekima hii na miujiza hii? Huyu si mwana wa seremala?” Tunaomba kwa sala
zako, uwabariki na kuwatia moyo mafundi seremala wote ambao kazi zao ni sawa na
ya kwako. Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA TANO
Mt. Yosefu,
Mwenyeheri, mume wa Bikira Maria, uwe nasi katika siku hii ya leo. Ulimlinda na
kumthamini Bikira Maria. Ukimpenda mtoto Yesu kama mwanao wa kumzaa, ulimwokoa
kutoka katika hatari ya kifo. Ulilinde Kanisa, nyumba ya Mungu, lililokombolewa
kwa damu ya Yesu. Mlinzi wa familia Takatifu, uwe nasi katika majaribu.
Tunaomba utuombee tujaliwe nguvu ya kuziepuka dhambi na kuzishinda nguvu za
dhambi ili katika maisha tuweze kukua katika utakatifu na baada ya kufa,
tuvikwe taji la ushindi na kufurahia milele na milele. Amina.
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA SITA
Ee Mt. Yosefu, ambaye ulinzi wako ni mkubwa, wenye
nguvu na wa haraka mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, tunakukabidhi mahitaji na
haja za mioyo yetu. Ee Mt. Yosefu utusaidie kwa maombezi yako yenye nguvu na
utuombee kwa Mungu atupatie Baraka zote za kiroho kwa njia ya Bwana wetu Yesu
Kristo, ili kwa nafasi yako Mbinguni tuweze kumsifu na kumheshimu Baba Yetu wa
milele. Ee Mt. Yosefu, kamwe hatutachoka kukufikiria wewe ukiwa umembeba Yesu,
akiwa amelala mikononi mwako. Hatuthubutu kumsogelea akiwa amepumzika hivyo
karibu na moyo wako. Tunakuomba umguse kwa kwa niaba yetu, umbusu, umuombe nae
atubusu wakati tutakapovuta pumzi yetu ya mwisho. Mt. Yosefu, msimamizi wa
wanakufaa, utuombee. Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA SABA
Ee Mt.Yosefu, mfano wa wote
wanojituma kufanya kazi, utujalie neema ya kufanya kazi kwa moyo wa toba kwa
malipizi ya dhambi zetu nyingi; kufanya kazi kwa bidii kwa kuweka mbele upendo
wa kufanya kazi; kuliko vionjo vyetu; kwa shukrani na furaha, kuona ni heshima
kutumia na kukuza zawadi tulizopewa na Mungu, kwa njia ya kufanya kazi kwa
utaratibu, amani na kwa kiasi na uvumilivu, pasipo kulegea kwa uchovu, au ugumu
wa kazi; zaidi ya yote, kwa nia njema kabisa na kujikana wenyewe, tukikumbuka
daima kifo na maelezo tunayotakiwa kuyatoa kwa muda tuliopoteza, talanta
tulizofukia, mema amabyo hatujayatenda na kujiona sana katika mafanikio, kitu
ambacho ni hatari katika kazi ya Mungu. Yote kwa Yesu, Yote kwa Maria, yote
kufuata mafano wako, ee Baba wa imani Mt. Yosefu! Hii itakuwa ndio kaulimbiu
yetu maishani mwetu na milele.
Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA NANE
Ee Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika
masumbuko yetu; na kisha omba shime ya Mchuma wako mtakatifu tunaomba pia kwa
matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira mtakatifu
mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie
kwa wema siye tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tukakombolewa kwa damu yake.
Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako. Ee mlinzi amini wa
jamaa takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristo. Ee baba uliyetupenda
mno tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu
mwezaji, utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu
wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa mtoto Yesu katika hatari ya
kuuawa, na leo hivi likinge kanisa takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na
katika shida yote, Mtunze daima kila mmoja wetu kwa mfano wako, ili tupate
msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni
makao ya raha milele. Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SIKU YA TISA
Mt. Yosefu, ututazame, sisi tuliyekuchagua wewe leo
hii uwe msimamizi watu wakati wa uhai wetu na katika saa ya kufa kwetu.
Ututazame na kutu zidishia moyo wa sala na wa kumtumikia Mungu. Ufukuze mbali
nasi kila aina ya dhambi, utuombee ili kifo kisitujie tukiwa hatujajiandaa,
bali tupate muda wa kutubu dhambi zetu zote kwa njia ya sakramenti ya kitubio
katika hali ya majuto kamili, ili saa ile ya kufa kwetu tukabidhi roho zetu
mikononi mwa Yesu na Maria. Amina.
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako,
tukiomba kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa
taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salaam Maria x 3 Atukuzwe
Baba x 3
SALA YA MWISHO
Ee bwana wetu Yesu kristo, tunaleta maombi yetu
maalum kwako ingawa hayatimizi kamwe kwa ukamilifu mahitaji yetu na matamanio
mengi yaliyomo moyoni mwetu. hatuombi kutimiziwa tu maombi yetu hayo bali Neema
ya kukutegemea wewe katika kutimiza kiu ya mahitaji na matamaniao ya mioyo yetu
ulivyotupatia wewe. Tunakuomba Bwana Yesu ujibu sala na maombi ya waja wako
walioungana nasi katika kusali Novena hii. Tunakuomba uwabariki kwa pendo lako
na uwatakatifuze. Tunakuomba kwa mioyo yetu iliyo wazi kabisa tukijua kuwa
haitatufaidia chochote tukivipata vya ulimwengu huu na kuipoteza nafsi zetu. Ee
bwana Yesu Kristu, tusaidie daima kuona wema na utukufu wako katika majaribu
yetu yote. Tusaidie pia kuona Baraka zako kila siku na daima kukupenda zaidi na
zaidi. Asante bwana Yesu kwa kila kitu kwetu. Amina.

Post a Comment