NOVENA KWA MT. RITA WA KASHIA
Makala hii inahusu mwongozo wa sala kwa siku tisa za novena ya Mt. Rita wa Kashia na siku tatu za Shukrani
SIKU YA KWANZA
Kwa jina la Baba,na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee Mtakatifu Rita mfanya miujiza, uniangalie kwa macho yako
yenye huruma, mimi ninaye teseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka
damu umezungukwa na miiba. Yaone macho yangu, ee Mtakatifu Rita, kuwa hayatoki
machozi tena kwani machozi mengi yamenitoka.
Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate
tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu? Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima
unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na
mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu wa jina hilo, kwa kunijalia
toka kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba hitaji
lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Kila mtu anasifia utakatifu wako. Kila mtu anasimulia
maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa njia yako. Je,mimi tu nitakataliwa na
kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uniombee kwa Bwana Yesu ili
anionee huruma na kunisaidia katika masumbuko na mahangaiko yangu. Kwa maombezi
yako, Ee Mtakatifu Rita, niweze kupokea kile ambacho moyo wangu unatamani sana.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya
maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi,
bubu na viwete, watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhi na moto havina
nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi,
bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi: Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia
kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA PILI
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita wa Kashia. Naona njia ya
maisha yako imejaa majaribu na miiba mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua
moyo wako vipande vipande. Ee Rita uliye kweli shahidi wa maumivu makali.
Uliyeonja tone kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu makali.
Nafikiria juu ya moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa
maombezi yako (hapa omba hitaji lako unalotaka
kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Wewe unajua maana ya moyo unaovuja damu. Unajua pia kifodini
cha roho. Umeumizwa sana na kuteseka sana. Kwa njia ya mateso hayo nakuomba
unisaidie katika mahangaiko yangu. Je, si kweli kwamba wakati huu mgumu, Bwana
wetu Yesu ametuandalia njia ya kujipatia neema kupitia miujiza ambayo binadamu
wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi yako wakafanikiwa?
Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie roho iliyopondeka inayolia na
kuhuzunika mbele yako. Ninakutumainia, Ee Mtakatifu Rita. Niombee kwa Yesu
mbinguni ili nipate kupokea yote ninayomwomba Mungu kwa maombezi yako yenye
nguvu.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita: homa, madonda na tauni, viini
vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu,
viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina
nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo
yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi,
bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako
Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema,
hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la
uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za
kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo
ulilotuahidi kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele.
Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA TATU
Kwa jina la Baba,na la Mwana,na la Roho Mtakatifu. Amina
Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa mapumziko, huku
macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii
hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu, najiona nimepotea kabisa.
Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Ritha, unaye ng’ara kama nyota inayoangaza kwa
mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za kanisa katoliki, natambua wewe
unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa
uchungu. Ninakuamini, kwa hamu nangojea, kupata kile nikiombacho
(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)
Nifikishie ombi langu kwa Yesu wa msalaba. Nakumbuka kipindi
kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopata majaribu,kwa utii ulipokubali
kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo
ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka
yako ya kishujaa, uliyomtolea Mungu wana wako,ukiomba wasinajisiwe kwa dhambi. Uniombee
kwa Mungu. Hicho ni kifo dini cha moyo wako. Kupitia mateso ambayo Bwana Yesu
kristo aliruhusu yakupate ili utakaswe katika majonzi yako, kwa njia ya
majiribu mengi yaliyokupata na sadaka nyingi ulizotoa, uniombee ili nijaliwe
kupewa ombi langu ninalongojea kwa hamu.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya
maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA NNE
Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Ee Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana, na wakili wa
waliokata tamaa. Hizi ni sifa safi zenye kujaa tumaini kwa roho zenye
kujaribiwa na uchungu. Kwako wewe Mtakatifu Rita wa kashia, ambaye wakati
tunapojikuta pweke katika maisha yetu, tunapozungukwa na huzuni na kifo, wewe
watujia kama mtunza bustani kutoka mbinguni kutuletea ndani ya mioyo yetu
iliyokauka tumaini na maji yaliyo hai.
Ee tumaini la moyo wangu ulikauka kutokana na msongo mkubwa
wa huzuni; uzito wa maafa umenielemea, mashaka yananiogofya na sijui nielekee
wapi kutafuta msaada ninaohitaji. kwako wewe Rita mwema, ninakuamini sana na
kukutegemea; nakujia nikiwa na uhakika utanisikiliza. Kwa nguvu ya maombezi
yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, natumaini kusikilizwa katika ombi langu
(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu
kupitia Mtakatifu Rita)
Jionyeshe tena kuwa u mwenye nguvu na huruma. Nithibitishie
pia kuwa ni kweli kama wafuasi wako wanavyokukili kuwa Mtakatifu wa yale
yaliyoshindikana, na wakili wa waliokata tamaa.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya
maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA TANO
Kwa jina la baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ewe mchumba mpendwa wa Yesu, Mtakatifu Rita wa Kashia;
nakuja kwako tena. Nipo miguuni pako. Navutwa na wema wako kwa Roho zenye
kutaabika na kusumbuka. Unaona moyo wangu ulivyo pondwa pondwa kwa magumu ya
dunia hii. Sipati tena tabasamu la thamani, Roho yangu imevamiwa na mashaka
mabaya. Imani imetetereka na mshituko wa kukata tamaa kama msituko wa kifo
unapiga miayo miguuni pangu. Nielekeze, Ee Mtakatifu mpendwa nifanye nini
katika mazingira haya ya kutisha? Nishauri nimwendee nani katika hali ya hatari
katika maisha yangu.
Kama kweli wewe ni Mtakatifu wa hali zote za kukatisha
tamaa, njoo unisaidie kwani najisikia nimepotea. Nakuja kwako wewe ambaye kila
mara wawahurumia wanaoteseka. Nakuja kwako unisaidie. Je, hutanionea huruma
kutokana na hali yangu? Mtakatifu Rita najua u mwema sana. Najua hivyo, ndio
maana najiweka mikononi mwako kwa moyo wangu wote ili unijibu kwa njia ya Yesu,
lile ombi langu ambalo kwa imani naliomba (hapa
omba hitaji lako unalotaka kunwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya
maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA SITA
Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Nafahamu kwa sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa
na wingu zisiweze kufika katika kiti chako cha enzi. Dhambi zangu ni sababu ya
adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri wa kuelekeza sauti yangu kwa Yesu, kwa kuwa
mara nyingi sikuthamini huruma yake. Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki.
Mkono wake wa haki umenielekea. Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha
wake kwani nimegubikwa na huzuni kubwa. Pasipo na matumaini nayalilia madhambi
yangu.
Niambie Mtakatifu Rita, Je, niendelee kukata tamaa? Hapana.
Bwana wetu Yesu Kristo amekuteua kuwa mtetezi wake mwenye nguvu ili uniombee
kwa Yesu wangu aliye juu, msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia safi ya kutotenda
dhambi tena.
Kwa uamuzi huu
thabiti,wa midomo yangu na moyo wangu, nakuelekea wewe. Eee Mtakatifu mtenda
miujiza, uniombee kwa Bwana Yesu fadhila ambazo nazihitaji sasa (hapa omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita).
Katika muda huu wa uchovu mkubwa, huzuni na kuachwa pweke,
Ee Rita, neno lako kwa Yesu litafungua huruma na msamaha wake. Sema neno na
Yesu atakusikia.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA SABA
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee mpedwa Rita, ambaye maisha yako yalikuwa ya huzuni.
Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu makali. Naomba sala zangu,
uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo wako mpole ili uweze
kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote uliionesha kwa Jirani,
maneno ya amani na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa watu wote vinivute
kukuelekea wewe uliye katika mbingu na unakoishi na kuwa mwombezi wa watu wote
waliokata tamaa.
Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo kinarudi nyuma, vipofu
wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza wanaponyeshwa na ulemavu wote wa
roho na mwili unaondoka kabisa. Je! Nipo peke yangu nisiyefarijiwa na maombezi
yako? Sitaamini wala siwezi kuamini hivyo. Naam, naamini kwa dhati usimamizi
wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Nina matumaini makubwa
kuwa nitapata amani moyoni mwangu, utulivu na fadhila ninazoomba nitajaliwa, (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita)
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA NANE
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona
ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana, ninapotafakari paji la uso
wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka katika taji la miiba la Yesu Kristo,
mchumba wako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni
mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake
akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa.
Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako, na
nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati
mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako.
Naamini sala hii kwako wewe mama mpenzi sana haitapotea bure.
Wewe uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni,
unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo
lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita).
Mungu hakukatalii wewe kitu chochote; kwa maombezi yako, miujiza
hufanywa, neema na fadhila maalumu hupatikana. Hivyo, kwa moyo wangu wote na
matumaini ya dhati, ninasubiri nikitegemea kupata haya niliyoomba kwa Bwana
Mungu.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
NOVENA SIKU YA TISA
Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Nina kuja mbele yako, Ee Mtakatifu Rita, siku hii ya mwisho
ya Novena hii Takatifu. Ninayasikia mapigo ya moyo katika kipindi hiki kigumu
cha maisha yangu yaliyogawanyika. Ninaamini kwamba ombi langu litatimizwa na
Bwana kupitia maombezi yako Matakatifu. Lakini ikiwa haiwezekani, ninapaza
sauti nikiomba kwa nguvu huruma na faraja yako. Usiniache niondoke bila kupata
faraja yako.
Ee Mtakatifu Rita, ninaomba unifariji kwa mastahili ya
mateso uliyoyapata hapa duniani na katika upweke wako wa sala. Unifariji kwa
mastahili ya ukarimu uliokua nao kwa wenye shida unisikilize kwa kwa mastahili
ya upendo wako mkuu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa mama yake Bikira Maria
Mtakatifu asiye na doa. Kwa mastahili ya ule mwiba Mtakatifu aliokujalia Bwana
wetu Yesu Kristo, unisaidie na unifadhili mimi.
Hiki ndicho kilio changu cha mwisho kwako wewe mama uliye;
Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa. Ninakuomba
ujidhihirishe katika mwanga wako halisi, ili Mungu anijalie haya ninayo yaomba. (hapa omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita)
Kwa msaada wako ninadhamiria kuachana na mwenendo wangu
potofu, ili niwe muenezaji wa nguvu za Mungu na uzuri wa mambo ya Mbinguni.
Ninaahidi pia mahali pako pa upweke, Ee Mtakatifu wa sala, huko Kashia, na (au)
kwenye sanamu yako: ili niweze kuungana nawe katika kuabudu na kushukuru kwa
fadhila za Mbinguni nilizozipata kwa maombezi yako kutoka kwa Mwokozi wetu
Azizi Yesu Kristo.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo
yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
SHUKRANI KWA HESHIMA YA MAOMBEZI YA MTAKATIFU RITA WA
KASHIA
SIKU YA KUMI (Siku ya
kwanza ya shukrani)
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Baba wa milele! Ambaye huruma yako haina mwisho, na wema
wako ni wa milele. Niangalie nikikusujudia kwa unyenyekevu mbele ya kiti chacko
cha Enzi kitukufu. Nainua kutoka chini ya moyo wangu utenzi wa kukushukuru kwa
upendo ulionijalia kupitia mtumishi wako Rita wa Kashia. Natambua eeh Mungu
wangu kuwa sistahili kupata fadhila ulizonikirimia na kwa kutokujali mapungufu
yangu bali umenisikiliza sala yangu kwa maombezi ya mtakatifu Rita wa Kashia.
Ee mtakatifu Rita mfanya miujiza maarufu wa kanisa katoliki;
kwako ninakutolea shukrani zangu za dhati. Kinywa changu hakina maneno ya
kutosha ya kueleza jinsi ninavyojisikia moyoni mwangu. Ee mtakatifu mpenzi, ni
kweli kwamba wote wanaotumainia maombezi yako hawakatishwi tamaa. Nijaze daima
neema ambayo naweza kupata kupitia huruma ya Mungu na unijalie ulinzi wako
katika maisha na kifo.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
SIKU YA KUMI NA MOJA (Siku
ya Pili ya Shukrani)
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee Moyo mpendelevu wa Yesu, ulio daima na utajiri na ukarimu
wa huruma isiyo na mwisho. Na ambaye ulimwambia nabii kuwa sikifurahii kifo cha
mtu mwovu bali ageuke na kuishi, uniangalie katika unyonge wangu.
Nakushukuru wewe kwa moyo wangu wote na kwa neema za pekee
ulizonijalia kupitia fadhila za mtumishi wako mteule, Mtakatifu Rita wa Kashia.
Je? Nitakurudishia nini, Ee Bwana, kwa upendo ulionijaloa? Ee Mungu wangu
sitaacha daima kukushukuru Wewe ambaye daima umekua mwema kwa wote
wanaokudharau.
Nawe mpenzi Mtakatifu Rita, nikulipeje fadhila ulizonijalia?
Moyo wangu umejaa furaha isiyo kifani. Nitakushukuru bila mwisho. Ee mtakatifu
mwema, uliye karibu na Bwana wetu; nipelekee Shukrani zangu kwake na kwako na
kuwa daima nitaichukia dhambi ili niendelee kufaidi huruma yake na maongozi
yake ya mbinguni.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo
yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
SIKU YA KUMI NA MBILI (Siku
ya tatu ya shukrani)
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ee Mungu wangu mpendwa, ambaye huwaachi wanye kukutumaini na
wenye kukuamini wapate mateso, bali kwa upendo wasikiliza sala zao. Toka
kilindini mwa moyo wangu nakutolea shukurani zangu za daima kwa fadhila
ulizonijalia kwa maombezi ya mtumishi wako uliyemchagua; Mt. Rita wa Kashia.
Pokea, Ee Bwana Yesu, shukrani zangu za dhati, zitokazo kama harufu nzuri ya
sadaka. Pokea kupitia mikono ya Mt. Rita. Ee Yesu mpenzi, nisaidie ili daima
niwe macho kupokea ukarimu wako, wema wako na huruma yako
Pamoja nawe, Ee Mtakatifu mtenda miujiza, ambaye jina lako
linatukuzwa kwa furaha kubwa duniani kote na ambaye maombezi yako huleta
miujiza; pokea shukurani zangu toka kilindini mwa moyo wangu. Ningetamani kila
mtu akujue; watu wote wakupende. Kwani watu wote wangetambua nguvu zako za
mbinguni
Ee nyota angavu ya Shirika la Mt Augustino; katika kutoa
shukurani kwa mema niliyopata kwa fadhila nyingi, nitaeneza kwa watu wote ibada
yako; nikiwaambia watu kuwa wewe kweli ni Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana,
mwombezi wa walio kata tamaa, mwombezi wa wote waliopoteza matumaini ya dunia
hii
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa,madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako; radi, tetemeko la ardhina moto havina
nguvu. kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo
yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako
unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata
akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso
alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe
adui zetu na kutafakari maumivu ya meteso yako, ili tupate tuzo uliotuhadia kwa
wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala daima na milele Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
LITANIA KWA MT. RITA WA KASHIA
Bwana utuhurumie, Bwana utuhurumie.
Kristo utuhurumie, Kristo utuhurumie.
Bwana utuhurumie, Bwana utuhurumie
Baba wa Mbinguni Mungu; Mwana Mkombozi wa Dunia Mungu; Roho
Mtakatifu Mungu; Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja; Kiitikio
“utuhurumie”
Maria Imakulata Mama wa Mungu; “Utuombee”
Maria mama mfariji wa wanaoteseka; “Utuombee”
Maria malkia wa watakatifu wote; “Utuombee”
Maria mwombezi mpenzi wa Mt. Rita “Utuombee”
Mt. Rita zawadi toka Mbinguni “Utuombee”
Mt. Rita mwombezi wetu mwenye nguvu; “Utuombee”
Mt. Rita uliyejaliwa Utukufu; “Utuombee”
Mt. Rita mstaajabiwa tangu utoto wako; “Utuombee”
Mt. Rita mpenda upweke; “Utuombee”
Mt. Rita kielelezo cha usafi wa moyo; “Utuombee”
Mt. Rita kielelezo cha upole wote; “Utuombee”
Mt. Rita kielelezo cha mke mwema; “Utuombee”
Mt. Rita kielelezo bora cha mama mtaratibu; “Utuombee”
Mt. Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli; “Utuombee”
Mt. Rita kielelezo hai cha kujikatalia; “Utuombee”
Mt. Rita kioo cha maisha ya kitawa; “Utuombee”
Mt. Rita kioo cha utii; “Utuombee”
Mt. Rita mvumilivu wa kustajabiwa; “Utuombee”
Mt. Rita shujaa wa kujitoa sadaka; “Utuombee”
Mt. Rita shahidi katika kufanya toba; “Utuombee”
Mt. Rita mjane mtakatifu; “Utuombee”
Mt. Rita, mkarimu kwa masikini; “Utuombee”
Mt. Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu; “Utuombee”
Mt. Rita aliyeingizwa utawani kimuujiza; “Utuombee”
Mt. Rita harufu nzuri ya manemane; “Utuombee”
Mt. Rita bustani ya kila fadhila; “Utuombee”
Mt. Rita mpendezwa na Yesu Msulubiwa; “Utuombee”
Mt. Rita uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso; “Utuombee”
Mt. Rita binti mpendevu wa Bikira Maria; “Utuombee”
Mt. Rita mwenye kiu ya upendo wa Kimungu; “Utuombee”
Mt. Rita uliyevikwa utukufu; “Utuombee”
Mt. Rita lulu ya mbinguni; “Utuombee”
Mt. Rita utukufu wa shirika la Mt. Augustino; “Utuombee”
Mt. Rita tunu ya thamani ya Umbria; “Utuombee”
Mt. Rita mwenye nguvu za utakatifu; “Utuombee”
Mt. Rita msamaha wa wanaopata mahangaiko; “Utuombee”
Mt. Rita mfariji wa wanaoteseka; “Utuombee”
Mt. Rita nanga ya wokovu; “Utuombee”
Mt. Rita mwombezi wa wagonjwa; “Utuombee”
Mt. Rita mwombezi wa mambo yaliyoshindikana; “Utuombee”
Mt. Rita kimbilio la walio hatarini; “Utuombee”
Mt. Rita msaada wenye nguvu kwa wote; “Utuombee”
Mt. Rita mastaajabio ya ulimwengu; “Utuombee”
Mt. Rita uliyepokewa mbinguni kwa furaha; “Utuombee”
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za ulimwengu, “Utusamehe
ee Bwana” Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za ulimwengu, “Utusikilize ee Bwana”
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za ulimwengu, “Utuhurumie”.
Kiongozi: Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: Kwa mhuli wa upendo na mateso
TUOMBE:
Ee Mungu, ambaye katika wema wako wa daima, umependa
kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale
ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka,
uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa
wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana
wetu. Amina
Kila baada ya kusali novena ya siku, tunasali litania hii kwa siku zote 12
Mt. Rita wa Kashia... utuombee

Post a Comment