WATAKATIFU ANNA NA JOAKIMU



HISTORIA.

Mtakatifu Anna ni Mtakatifu aliyemzaa Mama Bikira Maria pamoja na mmewe Mtakatifu Joakimu. 

Jina Anna likitoka kwenye Kiebrania Hannah, yaani "fadhili".

Mtakatifu Anna anaheshimiwa kama mama wa Bikira Maria na bibi wa Yesu, ingawa hatajwi katika Biblia, isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo kadiri ya Maandiko.


IBADA YA WATAKATIFU JOAKIM NA ANNA.

Ibada na heshima kwa watakatifu Joakim na Anna wazazi wake Bikira Maria ni mwendelezo wa Ibada kwa Bikira Maria na hatimaye, Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu. 

Matukio yote haya yanapaswa kuangaliwa katika mwanga wa Maadhimisho ya Mwaka wa Furaha ya Upendo Ndani ya Familia, “Famiglia Amoris Laetitia.” ili kuboresha sera na mikakati ya tunu msingi za familia!

Baba Mtakatifu Francisko anasema, huu ni muda muafaka wa kuanza kuvuna matunda yaliyopatikana katika kipindi na nyakati mbalimbali za maisha


MAFUNDISHO

Familia inapaswa kusimikwa katika upendo wenye huruma, kwa kutambua kwamba, familia ni Kanisa dogo la nyumbani kwan wazazi wake Bikira Maria, wanaonesha umuhimu wa familia kama shule ya upendo, imani na utakatifu wa maisha

Wazazi na walezi wanayo dhamana kubwa ya kuhakikisha kwamba, wanajenga na kudumisha misingi ya imani kama sehemu ya mchakato wa ukomavu wa imani miongoni mwa watoto wao.

Wazazi na walezi warithishe imani hii kwa njia ya maneno, lakini zaidi kwa njia ya ushuhuda wa maisha adili na matakatifu; watoto wasaidiwe kupata mwanga na ufunuo wa Mungu katika maisha yao.

Wazazi wawasaidie watoto wao kutambua na kuthamini zawadi ya maisha inayopaswa kulindwa tangu pale mtoto hadi mauti inapomfika kadiri ya mpango wa Mungu.



Post a Comment

Previous Post Next Post