MTAKATIFU INYASI WA LOYOLA, PADRE NA MWANZILISHI WA SHIRIKA
HISTORIA YA MAISHA YAKE.
Inyasi alizaliwa mwaka 1491 huko Loyola (Hispania ya Kaskazini). Wazazi wake walikuwa matajiri, wakajaliwa kupata watoto kumi na mmoja, watatu wakiwa wa kike wa wanane wa kiume, Inyasi ndiye aliyekuwa kitindamimba.
Katika ujana wake aliingia kazi ya uaskari, akapigana kwa uhodari na maadui wa nchi yake. Walipokuwa karibu kuuteka mji wa Pampeluna, alipigwa risasi mguuni. Akapaswa kulala kitandani kwa siku nyingi ili mguu wake upane kupona. Aliudhika sana kwa maana hakuwa na kitu chochote cha kufanya hapo kitandani kutwa kucha.
Mwishowe aliomba kitabu cha kusoma, akapewa vitabu vya Maisha ya Yesu na Maisha ya Watakatifu. Baada ya muda, alipata kutambua kwamba ujasiri wa kweli unapatikana katika kuufuata mfano wa Watakatifu kuliko katika ushujaa wa kijeshi. Nia ya Inyasi sasa ilikuwa kumtumikia Yesu Mfalme.
MAISHA YAKE YA UTUME KAMA MTAKATIFU.
Alianza kufikiri juu ya maisha yake ya kiroho. Mambo hayo yalichukua muda, wala hayakuendelea bila matatizo. Siku moja Bikira Maria alimtokea na mara mashaka yake yalikwisha. Alijitolea mwili na roho kwa Yesu akiapa kumtumikia mpaka kufa kwake, atakuwa askari wa Kristo, na kufuata matendo ya ujasiri wa Watakatifu.

Inyasi alipopona alienda katika Kanisa la Monte Serat, akaungama dhambi zote alizotenda tangu kupata akili. Alivua mavazi ya Kiaskari, akautundika upanga wake kwenye altare ya Bikira Maria. Alijificha muda wa mwaka mzima pangoni mwa Manresa akisali na kufunga kutwa.
Hapo ndipo alipoandika kwa uongozi wa Bikira Maria kitabu kile bora kiitwacho *'Mazoezi ya Kiroho'.* Watu wengi wamepata kuongoka na kupata utakatifu kwa kufuata mashauri yaliyoandikwa humo. Kisha kumaliza mafungo ya mwaka mzima huko Manresa, alienda kuhiji Yerusalemu. Aliporudi alijifunza muda wa miaka sita, akianza na Sarufi ya Kilatini kwenye shule ya Wavulana ya Barselona (Hispania).
Wakati ule Inyasi alikuwa na umri wa miaka 33. Baadaye alisoma Teolojia katika Chuo Kikuu cha Paris (Ufaransa). Alipokuwa na umri wa miaka 47, alipata Upadre huko Roma, akamaliza mwaka mzima akijitayarisha kwa Misa yake ya Kwanza.
Huko Paris alikutana na Mtakatifu Fransisko Ksaveri na vijana wengine. Akiwa na hao vijana, Inyasi alianzisha Shirika la Wajesuiti au "Chama cha Yesu". Wajesuiti hao waliweka nadhiri ya kwenda popote watakapotumwa na Baba Mtakatifu wa Roma. Walifaa sana kwa kusitawisha dini Katoliki katika nchi zote. Hata siku hizi bado wanashindana na maadui wa Kanisa Katoliki kila mahali duniani. Ndiyo maana watu wabaya wanawachukia, hata pengine wanajaribu kuwafukuza. Mtakatifu Inyasi na Mapadre wa Shirika lake huzoea kusema: "Tutende vitu vyote ili Mungu apate kusifiwa zaidi na zaidi".
Inyasi wa Loyola alifia huko Roma mwaka 1556. Pamoja na Fransisko Ksaveri aliandikwa katika orodha ya Watakatifu mwaka 1622.
MT. INYASI WA LOYOLA, UTUOMBEE

Post a Comment