Masomo ya Misa 14/10/2024

Somo la Kwanza

Gal 4:22-24, 26-27, 31:5:1

Imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili.Mmoja alikuwa mjakazi na mwingine alikuwa muungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa muungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, mmoja kutoka Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni hajiri. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, furahi wewe uliye tasa, usiye zaa; paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu:maana watoto wakealiyeachwa pekee ni wengi kuliko huyo aliye na mume. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazibali tu watoto wa huyo aliye mwungwana. Katika ungwana huo Kristo alituandikia huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu 

Wimbo wa Katikati

Zab 113:1-7

Aleluya

Enyi watumishi wa Bwana sifuni

Lisifuni jina la Bwana

Jina la Bwana lihimidiwe

Tangu leo na hata milele.

(K)Jina la bwana lihimidiwe milele

Toka mawio ya jua hata machweo yake

 Jina la bwana husifiwa

Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote

Na utukufu wake ni juu ya mbingu

(K)Jina la bwana lihimidiwe milele

Ni nani aliye mfano wa bwana

Mungu wetu aketiye juu

Anyenyekeaye kutazama

Mbinguni na duniani?

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini

Na kumpandisha masikini toka jaani.

(K)Jina la bwana lihimidiwe milele

Shangilio

Zab 119:34

Aleluya, aleluya

Unifahamishe nami nitaishika sheria yako

Nitaitii kwa moyo wangu wote

Aleluya

Somo la Injili

Lk 11:29-32

Makutano walipokuwa wakimkusanyikia, Yesu alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka nchi za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.

Neno la Bwana, Sifa kwako Ee Kristu 

Post a Comment

Previous Post Next Post