Somo la Kwanza
Mdo 19:1-8
Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati
ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
akawauliza, Je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia
kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo
gani? Wakasema, kwa ubatizo wa Yohane. Paulo akasema, Yohane alibatiza kwa
ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani,
Yesu.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 68:1-6
Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika,
Nao wamchukiao huukimbia uso wake.
Kama moshi upeperushwavyo,
Ndivyo uwapeperushavyo wao;
Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,
Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
(K) Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu. au: Aleluya.
Bali wenye haki hufurahi,
Na kuushangilia uso wa Mungu,
Naam, hupiga kelele kwa furaha.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,
Shangilieni mbele zake.
(K) Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu. au: Aleluya.
Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu katika kao lake takatifu.
Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;
Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;
Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
(K) Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu. au: Aleluya.
Shangilio
Mt 28:19, 20
Aleluya, aleluya,
Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mimi nipo
pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari.
Aleluya.
Somo la Injili
Yn 16:29-33
Wanafunzi walimwambia Yesu: Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu.
Yesu akawajibu, Je! mnasadiki sasa? Tazama. saa yaja, naam,
imekwisha kuja ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke
yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. Hayo
nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini
jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Post a Comment