Maisha yake

Mtakatifu Augustino, alizaliwa mwaka 354 November 13 huko Tagaste, Numidia, (sasa Souk Ahras-Algeria ).Alikuwa mtoto wa Mtakatifu Monica,na Baba yake alikuwa mpagani.

Mtakatifu Agustino alisoma huko Tagaste, Carthage na Roma.Alifuata mafundisho mabaya,na kuingia katika maisha ya kidunia.

Mama yake alidumu katika sala,akimwombea abadilike katika mienendo mibaya. Na kutokana na elimu yake, Mtakatifu Augustino alipewa kazi mbalimbali ,huko Milan.

Mwaka 386,Mtakatifu Augustino aliamua kubadilika na kuwa mkristo. Alibatizwa mwaka 388 na Askofu Ambrose (Mtakatifu ) na mama yake alikufa siku chache baada ya ubatizo huo.

Mtakatifu Agustino alirudi Algeria, ambako aligawa mali zake,na nyumba yake ikawa makazi ya mapadre na watawa.

Mwaka 391 alipata daraja la Uaskofu, akawa Askofu wa Hippo.Kutokea hapo, akawa mhubiri mzuri,akaandika maandiko mengi na vitabu.Pamoja na nyaraka mbalimbali.

Mtakatifu Augustino alikufa mwaka 430,August 28, huko Hippo, Numidia (sasa Annaba- Algeria ) baada ya kuugua . Akatangazwa Mtakatifu mwaka 1298 na Papa Boniface VIII

Watakatifu wengine wa leo ni

Mt. Alexander wa Constantinople

M/h. Aurelio da Vinalesa

Mt. Edmund Arrowsmith

Mt. Facundius

Mt. Fortunatus

Mt. Gorman

Mt. Hermes

M/h. Hugh More

W/h. John Roche na Margaret Ward

Mt. Julian wa Auvergne

M/h. Laurentia Herasymiv

Mt. Moses wa Ethopia

Mt. Pelagius wa Constance

M/h. Robert Morton

Mt. Rumwald

M/h. Teresa Bracco

M/h. Thomas Felton

M/h. Thomas Holford

Mt. Vivian

W/h. William Dean

W/h. William Guntei

Mtakatifu Augustino, Wenye heri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee.

Post a Comment

Previous Post Next Post