MAISHA YA MTAKATIFU ELIZABETH BISHIYE (1838) MWANZILISHI WA SHIRIKA 

Elizabeth alizaliwa Ufaransa mwaka 1778, baba yake alikuwa mtu wa maana sana serikalini. 

Elizabeth alipokuwa na umri wa miaka kumi na Tisa baba yake alifariki.

Alijifunza sheria na hesabu Ili kuweza kuangalia na kutunza mali ya familia ujuzi huo ulimfaa baadaye.

Alipokuwa na miaka ishirini na minne aliandika nyuma ya picha ya Bikira Maria: " Mimi, Elizabeth Bishiye, leo najitoa mwenyewe kwa Yesu na Maria kwa Milele yote". 

Picha hiyo na maandishi ipo bado mpaka leo.

Wakati huo ulikuwa wakati wa mapinduzi ya Ufaransa na Mapadre walikuwa wanauawa sana. 

Elizabeth alizoea kukusanya familia mbalimbali Ili kusali, kuimba na kusoma neno la Mungu.


Alikuwa na uhusiano na Padre mmoja ambaye baadaye alikuwa Mtakatifu: Mtakatifu Furnet. 

Padre huyu alimkatisha Elizabeth tamaa ya kuingia Utawa, alisema: " Kazi yako iko duniani". 

Alimshauri aendelee na kazi yake kwa hiyo Elizabeth aliendelea kuwatembelea wagonjwa, wazee, masikini, na kuwafundisha watoto wadogo.  

Baadhi ya Marafiki zake walimsaidia katika shughuli hizi na baada ya kifo cha mama yake mwaka 1804, kikundi hiki kidogo cha Wanawake kilifanya nadhiri mnamo mwaka 1807, wakiitwa "Mabinti wa Msalaba".


Kwa muda wa miaka kumi na tano kikundi hiki kilianzisha nyumba sitini za Watawa katika Majimbo Mbalimbali. 

Mwaka 1836 Elizabeti aliugua na baada ya miaka miwili hali yake ilizidi kuwa mbaya.

Aliteseka sana lakini kwa uhodari alivumilia na alikufa kwa amani jioni ya tarehe 26 Agosti 1838.

Alitajwa Mtakatifu mwaka 1947.


MTAKATIFU ELIZABETI BISHIYE MWANZILISHI WA SHIRIKA, UTUOMBEE..

Post a Comment

Previous Post Next Post