HISTORIA YA MAISHA YA MTAKATIFU CARLO ACUTIS

Leo Septemba 07, 2025 Kanisa Katoliki likiongozwa na Papa Leo XIV limemtangaza rasmi Mtakatifu Carlo Acutis pamoja naye ni Mtakatifu Pier Giorgio Frassati.

Mtakatifu Carlo Acutis alizaliwa Mei 3, 1991 huko London na baadae alikulia na kupata malezi akiwa Milan, Italia kwa wazazi wake.

Alipata nafasi ya kujifunza program za kumpyuta ambazo zilimwezesha kutengeneza tovuti ambayo ilielezea zaidi kuhusu upekee, umuhimu, ukuu na mengine mengi kuhusu Ekaristi Takatifu.

Alifariki mwaka 2006 tarehe 12 Oktoba kwa ugonjwa wa Leukemia akiwa na umri wa miaka 15.

Safari yake kufika siku ya kutangazwa kuwa Mtakatifu ilianza mwaka 2013 alipotangazwa Mtumishi wa Mungu ambapo Jimbo lake la Assisi lilianzisha rasmi mchakato wa kuchunguza maisha yake.

Mwaka 2020 Oktoba 10, Papa Francis alimtangaza kuwa Mwenyeheri kufuatia miujiza iliyotokea huko Brazil mwaka 2013, inayohusishwa na maombi yaliyoombwa kupitia yeye.

Mei 23, 2024 Papa Francis alikiri muujiza ambao ulitokea kwa mwanamke wa Costa Rica, Valeria ambaye alipona baada ya maombi ya familia yake kwa Mtakatifu Carlo Acutis.

Awali ilipangwa kutangazwa Mtakatifu Aprili 27, 2025 kwenye Jubilei ya vijana huko Vatican, lakini ilisitishwa baada ya kifo cha Papa Francis aliyefariki katika Jumatatu ya Pasaka 2025.

Kisha hapo, Papa Leo XIV alikuja kutangaza tarehe rasmi ya kumtangaza Mtakatifu ambayo ni leo Septemba 07, 2025.

Kupitia maisha ya Mtakatifu Carlo Acutis, sote tunaalikwa kumwomba Mungu kupitia maombezi ya Mtakatifu huyu nasi tuwe na upendo mkubwa kwa Ekaristi Takatifu, tuweze kutumia vipaji vyetu kwa ajili ya Mungu, tuwe wanyenyekevu na tutoe huduma kwa maskini na tumweke Mungu kwanza katika maisha yetu ya kila siku.

Mtakatifu Carlo Acutis na Pier Giorgio Frassati.

Mtuombee....

Post a Comment

Previous Post Next Post