MTAKATIFU ROKO WA MONTPELLIER.
Alizaliwa mwaka 1348 huko ufaransa. Alikuwa mkristo maarufu kwa kuishi miaka mingi bila makao maalumu. Ndiyo maana kwa kawaida anachorwa amevaa nguo za hija.
Katika mizunguko yake sehemu mbalimbali aliwahudumia kishujaa waliopatwa na tauni na kuwaponya wengi kwa mkono wake wenye karama.
Miaka 3-5 ya mwisho alikuwa mfungwa gerezani akidhaniwa mpelelezi, asifanye chochote kwa kujitetea au kujitambulisha kwa watawala ambao walikuwa ndugu zake wakamtambua baada ya kufa tu.
Tangu kale ni kati ya watakatifu maarufu zaidi duniani, pia kwa sababu ya miujiza iliyosemekana alifanya wakati wa uhai wake na baada ya kifo, hasa kwa wagonjwa wa tauni, kama alivyoahidi kwa maandishi.
Sikukuu yake ni tarehe 16 Agosti ambayo ni siku aliyofariki mnamo mwaka 1379.
MT.ROKO WA MONTPELLIER,
UTUOMBEE.
Post a Comment