MT. PAPA HORMISDAS

Alikua papa kuanzia tarehe 20/7/514 akifuata baada ya Papa Simako na kufuatwa na Papa Yohane I. 

Alipochaguliwa alikua shemasi mjane kutokana na ndoa yake, alikuwa na mwana aliyekuja kuwa Papa Silverio baadae.

Aliwapatanisha waliokuwa wafuasi wa antipapa Laurentius na akafaulu pia kumaliza farakano lililoanzishwa na Patriarki Acacius wa Konstatinapoli. Tangu kale alihesabiwa kuwa mtakatifu.

Alifariki tarehe 6/8/523 na sikukuu yake hufanyika siku 6/8 kila mwaka.

MT. PAPA HORMISDAS,

UTUOMBEE.

Post a Comment

Previous Post Next Post