UPWEKE-UGONJWA
WA ROHO
INJILI:
YOHANE 5:1-9
Baada
ya hayo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea Kwenda Yerusalemu.
Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania
Bethzatha, nayo ina matao Matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa
walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao walopooza, (wakingoja maji yachemke. Kwa
maana wakati ambako Malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua
maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa
wote uliokuwa ummempata). Na hapo palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda
wa miaka thelathini na minne. Yesu alipomwona huyo amelala, naye akijua kuwa
amekuwa hali hiyo siku nyingi alimwambia, “Wataka kuwa mzima?”. Yule mgonjwa
akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila
wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.” Yesu akamwambia,
“Simama, jitwike godoro lako, uende.” Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika
godoro lake, akaenda.
Neno la Bwana ………
Tukitazama
katika somo la Injili tunamwona Yesu anakwea kuelekea Yerusalemu, hasa hasa
anaelekea Bethzatha (mlango wa kondoo) ambako kulikuwa na wagonjwa wengi na
wahitaji wa aina mbalimbali waliokuwa wakisubiri maji yatibuliwe waweze kuingia
kwenye birika ili kuponywa matatizo yao.
Jamii
hii haitambui uwepo wa Yesu katikati yao na wote wameweka umakini wao katika
zile birika tano wakingojea Malaika kushuka na kuyatibua mji yake. Lakini
katika msongamano wote huo wa wahitaji na wagonjwa Yesu anamwendea mmoja kati
yao.
Tazama
mazungumzo yao: -
Yesu
alipomwona huyo amelala, naye akijua kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi
alimwambia, “Wataka kuwa mzima?”.
Yesu
ingana anajua kuwa mgonjwa huyu amekuwa katika hali aliyokuwa nayo kwa siku
nyingi kuna swali la muhimu anauliza [wataka kuwa mzima], Yesu
analifahamu hitaji la mgonjwa huyu lakini anauliza tena juu ya hitaji hilo,
Yesu anajaribu kuipima Imani ya mtu huyu katika uponyaji amabo amekuwa
akiusubiri kwa kipindi kirefu. Yesu anaitafuta Imani ndani ya mtu huyu.
Waebrania
11:6 “lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.”
Kristu
anajaribu kuiangalia Imani ya mtu huyu ili aweze kumpatia thawabu ya uponyaji.
Twaweza kuwa kwa namna moja ama nyingine tuna hali saw ana ya mtu huyu nasi
twahitaji thawabu kutoka kwa Mungu, swali ambalo Yesu Kristu anapokuja kwetu
kutatua matatizo yetu ni sawa na la mtu huyu [wataka kuwa mzima]. Majibu
yetu ndio yatakayo hitimisha thawabu za Mungu kwetu sisi.
Lazima
tukumbuke
Marko
11:23-24 [amin, nawaambia; yeyote akatayeuambia mima huu, ‘Ng’oka ukatupwe
baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini hayo asemayo yametukia,
yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaabia; Yeyote myaombayo mkisali, aminini ya
kwamba mnayapokea, nao yatakuwa yenu.]
Hii
ndiyo ahadi ya Bwana wetu Yesu Kristu.
Tukiendelea
na mazungumzo ya Yesu na mtu yule tunaona: -
Yule
mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji
yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.”
Mtu
huyu mgonjwa anajibu tofuti na matarajio yetu sote, anamwambia [Bwana, mimi
sina mtu wa kunitia birikani…]. Mtu huyu mbali na kuwa katika hali ya ugonjwa
kwa kipindi kirefu kitu pekee anachokiona kma kikwazo ni UPWEKE, [mimi sina mtu
wa kunitia birikani].
Hali
hii ya upweke imekuwa I zaidi y ugonjwa kwa mtu huyu wa enzi zile lakini ni
tatizo la kiduni kwa nyakati za sasa. Wengi wetu tumekuwa tukilalama juu ya
kukosa mtu karibu yetu na tumekuwa tukimlilia Mungu juu ya swala hili, Mungu
tazama mimi sina mtu wa kunijali, sina mtu wa kuniangalia kwa ukaribu, sina mtu
nayeonesha upendo kwangu na mambo mengine mengi hatua ya kusahau hali zetu
tulizonazo.
Upweke
unaitafuna kwa kasi dunia ya sasa na watu wengi wanataza, wanahitaji baadhi ya
hali kama kupendwa, kujaliwa, kusikilizwa, kupewa msaada na mengine mengi na
yanapokosa haya watu huzama katika dimbwi la huzuni na Upweke huwatawala.
Katika
biblia agano la kale tunamuona Mungu wa Yakobo, Mungu wa Isak ana Mungu wa
waislaeli alikuwa juu ya watu wake akiwalinda kila pande, alikuwa juu yao kama
wingu lakivuli nyakati za jua kali na akawawakia kama nuru juu yao wakati wa
giza. Si hivyo tu, hata alipowavusha katika maji alikuwa pembeni yao
akiwalinda.
Je,
Mungu wetu yupo wapi katika dunia ya sasa, katika nyakati hizi za upweke, Mungu
yupo wapi?
Soma
simulizi hii
“Kando
ya ziwa kubwa waliishi jamaa wawili, mmoja Tajiri mtu aliyetunukiwa mali nyiki
kwa kadri alivyohitaji, naye alikuwa na mali sana na alikuwa amejenga bwawa la
kuogelea mbele ya nyumba yake. Pia alikuwepo jamaa mwingine, Jirani ya yule
Tajiri naye alikuwa wa kipato cha chini hakuwa na mali nyingi isipokuwa makazi
machakavu na pipa dogo la maji. Jamaa huyu maskini siku zote alikuwa akimchukia
jamaa yake aliyekuwa Tajiri na alikuwa akimlalamikia sana. Siku moja katika
malalamiko yake alimwambia, tazama wewe upon a bwawa la kuogelea na mimi nina
pipa moja dogo nyumabni kwangu, huna ukarimu wewe. Bwana yule aliyekuwa Tajiri
akamjibu akisema, Je! Wewe hauko pembezoni wa ziwa kubwa lililojaa maji,
kwanini usijitwalie kutoka humo kiasi utakacho kama mimi nilivyofanya”
Maisha
yetu yamekuwa saw ana jamaa maskini, tumekuwa tukilalamika na kusema kama yule
mtu mgonjwa [mimi sina mtu wa kunitia birikani,.]. na mara kwa mara tumekuwa
tukimuona Mungu kama katukimbia na kuondoka kutoka katika upeo wetu lakini
tunasahau kuwa Mungu yupo ndani yetu.
Kumbuka
Yohane
3:16 [Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uima wa milele].
Zama
zimebadilika, Mungu hayuko tena kukaa juu yetu kutuangazia, ama kukaa pembeni
yetu kutulinda, Mungu yupo ndani yetu, tunaishi naye, tunakula naye, tunalala
naye na kwa upendo waake huwa nasi ktika kila namna.
Mungu
anatuuliza ni kwa nini tunataza mambo na hali walizonazo wnzetu, na tunasahau
yale makubwa aliyotupatia sisi, Mwanawe wa pekee, Mungu ametupatia kila kitu
alicho nacho. Tunalalamika kila mara kuwa hamna mtu wa kutupenda, kutujali na kutusaidia
na kusahau kwamba Mungu anatupenda, anatujali na anaweza kufanya chochote kwa
ajili yetu.
Yohane
14:23 [Yesu akajibu akamwambia, “Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba
yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.]
Kwa
kumpenda Kristu situ kwamba Mungu atatupenda bali Mungu na mwanawe Yesu Kristu
watafanya makao ndani yetu, wataishi Pamoja nasi na watakaa nasi. ajabu gani
naya kushangaza bado tunalia juu ya kupendwa na watu wengine kuisahau hazina
iliyopo ndani ya Kristu.
Isaya
43:1-2 [ Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, ee Yakobo, “Usiogope, maana
nimekukomboa; nimekuitwa kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji
menginitakuwa Pamoja nawe, na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika
moto, hutateketea, wala mwali wa moto hautakuunguza.]
Mungu
yupo pamoja nasi katika hali zote za Maisha yetu, katika kukataliwa, katika
kupigwa na kudhalilishwa, yupo nasi katika mafuriko ya mkato wa tamaa na
maginjwa, katika moto wa umaskini na njaa, na sio kwamba anatutazama kutoka
mahali bali yupo Pamoja nasi. Tunapozama majini tunazama naye, tunapopita
motoni tupo naye, kwa maana huyo ndiye Mungu wetu.
Mungu
atakuwa nasi katika kila hali na atahakikisha kuwa tunatoka katika matatizo ytu
tulionayo si kwa ukombozi kamili bali kwa ushindi mkubwa. Tunaweza kuwa tumeona
moto wa aina mbalimbali, kimbunga kimeyatawanya Maisha yetu, mafuriko yamesomba
ndoto zetu na matumaini lakini tukumbuke kuwa Mungu nyakati zote yupo nasi.
Tufanye
nini sasa?
Isaya 41:10 [ Usiogope, kwa maana mimi ni
Pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, naam,
nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.]
Haya
ni maneno ya Mungu yanayoonyesha ahadi na agizo, sisi si wapweke, sisi si
yatima wala si watumwa, bali tu huru, wenye haki na baraka nyingi. Tumuamini
Mungu katika kila jambo kwani yeye yupo ndani yetu na katika Maisha ya kila
siku. Bwana anaisikia haja yetu, analijua hitaji letu naye hutuambia kila
nyakati [simama, jitwike godoro lako, uende.]
TUMSIFU
YESU KRISTU.....
Post a Comment