MT. DOMINIKO WA GUZMAN MWANZILISHI WA SHIRIKA LA WAHUBIRI.

Alizaliwa Hispania mwaka 1170 na kufariki Italia tarehe 6/8/1221. Na kanisa husherehekea sikukuu yake tarehe 8/8 kila mwaka.

Alikua padri wa kanisa katoliki na mwanzilishi wa shirika la wahubiri. Alikua mkanoni wa jimbo la Burgode Osma-Ciudad de Osma mwaka 1203 akiongozwa na askofu katika safari ya kibalozi kwa niaba ya mfalme. 

Kwa agizo la Mtaguso IV wa Laterano ndugu wa shirika walipaswa kuchagua kanuni iliyowahi kukubaliwa na kanisa wakaamua kushika ile ya Agostino wa Hippo maarufu haswa kwa kutumia kiasi fulani cha demokrasia ambayo ilitumiwa kama mwongozo kwa wengine hata za kiserikali.

Alitangazwa mtakatifu na Papa Gregori IX tarehe 2/7/1234. 

MTAKATIFU DOMINIKO WA GUZMAN,

UTUOMBEE.

Post a Comment

Previous Post Next Post