
Nini Maana ya Kilele cha Msalaba?
Kilele au Hitimisho au Maana halisi ya Msalaba ni PASAKA.
Bila Pasaka, Msalaba hauna maana yoyote (mateso bila ufufuko hakuna tija)
Faida za Msalaba
1. Unatusaidia Kutengeneza mahusiano binafsi. Yatupasa kujifahamu kwanza, ili kumfahamu Mungu (Hivyo tujifahamu kwanza.
2. Unatusaidia kutengeneza mahusiano bora wenzetu wanaotuzunguka.
3. Unatusaidia kutengeneza mahusiano bora na Mungu
Je, tutatengeneza vipi haya mahusiano katika kipindi hiki cha kwaresma?
Jinsi ya kuyatengeneza hayo mahusiano kupitia Kwaresma ni kwa
● Kufunga
● Kusali
● Kuomba
Yote haya tunafanya kuondoa mizizi ya dhambi ambayo ndio misalaba yetu.
Ni nini Maana ya Msalaba?
Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. (Lk 9:23)
Maana msingi ya msalaba ni KIFO.
Hapo awali kutoka kwenye historia ya maisha kabla ya kifo cha Yesu, msalaba ulikuwa ni chombo mahususi cha kuwaua waasi kwa lengo la kutaka jamii isirudie kosa hilo. Waasi hao walifungwa mikono yao katika misalaba na kusulubiwa njiapanda ili kila anayepita aweze kuwaona.
Lakini baada ya YESU kufa msalabani dhana ya msalaba ilibadilika, hivyo msalaba ukawa ni “ Kuifia dhambi iliyo ndani yako ili kuiacha.”
Mara nyingi tumekua tunaogopa kifo kwa sababu ya hali mbaya rohoni mwetu(wadhambi). Hiyo yatupasa kuwa wasafi, mioyoni mwetu na kuacha kuogopa kifo, kwani ni njia ambayo kila binadamu yampasa kuipitia. “Basi kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa (Mathayo 25:13)”
Kwaresma ndicho kipindi cha kujitafakari na kutafuta namna ya kuiondoa misalaba yetu (vilema vyetu). Mungu ametupa muda huu ili tubadirike ingawa shetani anatutia upofu wa kiroho na kutufanya tuyaone mambo ya ziada ndio ya muhimu. Yesu anatuhasa kuuvua urafiki mbaya kwenye mioyo yetu hasta kutoa sadaka kubwa. Tunahitaji uamuzi wa dhati wa kuyaondoa haya makandokandotuliyonayo, kwani “nafsi zetu ni za thamani sana”
Sehemu ya 2: Kufunga na Kwaresma
● Kufunga ni nini?
● Kwanini tufunge?
● Kuna uhusiano gani kati ya mfungo na kwaresma?
Rejea sehemu zifuatazo za maandiko Matakatifu:
"Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vilevile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie." Esta 4:16
Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi. Kutoka 34:28
Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. Danieli 9:3
Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia. Danieli 10:3
Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto; Daudi akafunga, akaingia, akalala usiku kucha chini. 2 Samweli 12:16
Kufunga ni nini?
Kufunga ni kujinyima na kujikatalia chakula na vinywaji (kwa maana ya kawaida).
Kufunga (Kikristo Kikatoliki) ni Kujikatalia/Kujinyima chakula na vinywaji ikiambatana na matendo ya kiroho ya kujirudi mwenyewe ili kupata neema za Mungu. Kufunga ni dawa nzuri ya kutuweka karibu zaidi na Mwenyezi Mungu
Ikiwa mtu ameamua kufunga, basi na afunge kweli. Kufunga ni kujinyima kabisa na sio kupunguza wingi wa chakula na vinywaji. Katika ukatoliki, kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu pamoja na uvivu na kujionea huruma juu ya miili yao kuteseka kwa kuumwa njaa, kanisa liliamua kuweka amri ya kufunga angalau suku moja katika kipindi cha kwaresma ambayo ni siku ya jumatano ya majivu. Kufunga Jumatano ya majivu ni amri na sio tena swala la mtu kuamua.
Binadamu ni muunganiko wa Mwili na Roho. Mungu kupitia malaika mlinzi (wa kila mmoja wetu) anawasiliana na roho zetu kwa njia ya Ndoto, Njozi, na wetu wa karibu yetu. Uchafu wa roho zetu unafarakanisha/ unakwamisha mahusiano ya Kiroho Kati yetu na Mungu. Tunapaswa kuzizingatia ndoto tunazoota na kutozichukulia kirahisirahisi na tumuombe Mwenyezi Mungu atufunilie juu ya ndoto na njozi hizo.
Faida za Kufunga(Kiroho)
1. Kufunga kunamuongezea mtu nguvu ya kiroho ya kupambana na maadui wa kiroho (sheteni). Kufunga ni kama booster ya kuongeza ushupavu na nguvu
2. Kufunga kunaongeza neema ya kujikwamua kutoka katika dhambi ili nafsi zetu ziwe huru na ziweze kuwasikiliza malaika wetu walinzi, wanaosema nasi hasa katika ndoto zetu
Dhambi hutufanya tushindwe kuelewa ujumbe wa Mungu anaotuletea kupitia malaika zake.
3. Kufunga kunasaidia kuweza kuutiisha mwili ili roho ziwe na nguvu kuliko miili yetu
Hii hutupata uwezo wa kuzuia miili yetu kuziendesha roho zetu na kuweka usawa kati ya miili yetu na roho zetu. Miili yetu ikitawala roho zetu, huyafunga macho yetu ya roho na kuona kila tukifanyacho ni sawa na daima kutotosheka maana tutatawaliwa na tamaa za macho ya nyama.
4. Kufunga husaidia kujifahamu sisi wenyewe na kuushinda ubinadamu wetu.
Shetani hataki mwanadamu afunge kwa sababu anajua kuwa atakua mnyenyekevu kama MUNGU anavyotaka tuwe na kwa sababu ya unyenyekevu tutafunuliwa neema na siri zake Mungu. (rejea: Isaya 42:3)
Mambo ya Kuzingatia
● Licha ya mazingira yetu yaliyojaa vishawishi wakati wa kufunga kwetu, Mfungo huanza na dhamira ya ndani kabisa na maandalizi ya akili ili kuepuka huo ushawishi wa kukufanya usitimize funga yako.
● Katika maisha yetu shetani hutupatia vitu ambavyo huonekana ni vizuri mno machoni na kusika vizuri mno masikioni mwetu. Mungu anatitaka tuwe na vitu vya kujitosheleza na sio kujilimbikizia mali hata kama hua hatuachi kuwasaidia wengine. Tunapaswa kuwapenda wenzetu kama tunavyojipenda sisi wenyewe.
● Tunaaswa kusali na kuomba. Hivi viwili huonekana kama vitu sawa lakini ndani yake hutoka maana mbili tofauti licha ya kwamba zote ni njia za kuongea na MUNGU. Kusali daima hubaki ndani ya akili tu (all about mental alone), kuongea na Mungu bila kuonesha juhudi zetu. Ila kuomba ni kusali na kutenda kwa kuweka na kuonesha juhudi ili MUNGU akujalie kadiri ya juhudi zako mwenyewe.
Post a Comment