MAFUNGU YA ROZARI
Matendo ya furaha (Jumatatu na Jumamosi)
- Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa mama wa Mungu, Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
- Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti, Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
- Yesu anazaliwa Bethlehemu, Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.
- Yesu anatolewa Hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
- Maria anamkuta Yesu Hekaluni. Tumombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Matendo ya uchungu (Jumanne na Ijumaa)
- Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu, Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
- Yesu anapigwa mijeledi kwa ajili yetu, Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
- Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu, Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
- Yesu anachukua msalaba kwa ajili yetu, Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
- Yesu anakufa msalabani, Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
Matendo ya utukufu (Jumatano
na Jumapili)
- Yesu anafufuka, Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu
- Yesu anapaa mbinguni, Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni
- Roho mtakatifu anawashukia Mitume, Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
- Bikra maria anapalizwa mbinguni, Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
- Bikra Maria anawekwa Malkia mbinguni, Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
Matendo ya mwanga (Alhamisi)
- Yesu anabatizwa Mto Yordani, Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
- Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana, Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya injili.
- Yesu anatangaza ufalme wa Mungu, Tumwombe Mungu atujalie kupokea ufalme wake kwa toba ya kweli.
- Yesu anageuka sura, Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
- Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi takatifu, Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
Tumsifu Yesu Kristo...
Post a Comment