Je, umewahi pata nafasi ya kusoma somo Kanisani? Je ulifanya kwa usahihi?

Mambo muhimu na baadhi ya kuzingatia katika usomaji

  • Msomaji anapaswa kujiandaa vizuri, si tu kufahamu kusoma, ila somo linapatikana wapi. Afahamu pia jinsi ya kurekebisha kipaza sauti. 
  • Ni vyema kuzingatia vituo katika kusoma na kunapokuwa na neno gumu, ni, heri kulirudia tena na tena ukiwa peke yako na kabla hujaenda kwenye Ambo (Mahala pa kusomea huitwa Ambo) kusoma.
  • Msomaji anapaswa kwenda kwenye ambo baada ya sala ya kolekta, (si sahihi kwenda wakati sala ya kolekta inasaliwa).  
  • Akifika mbele ya altare anapaswa kuinama kwa heshima, na kupiga goti moja kuelekea tarbenakulo (Kama hamna tarbenakulo hakuna haja ya kupiga goti).
  • Msomaji anapaswa kuvaa mavazi ya heshima.
  • Si sahihi kusoma aya na sura za somo husika.
  • Msomaji anapaswa kusoma kwa namna itakayowafanya waamini “wajenge mioyoni mwao upendo hai wa kufurahia utamu wa maandiko matakatifu” (UMMK 101).

Licha ya kupaswa kusoma vizuri: sauti ya kusikika, bila ya kumung`unya maneno wala kasi ya ajabu. Msomaji anapaswa kusoma somo husika mapema, hata siku moja kabla, na apate muda wa kulitafakari. Somo linapaswa kuwa la msomaji, lizungumze na yeye kwanza ili lipate kuzungumza na wengine kupitia yeye. Msomaji kamwe asikutane na Somo katika Ambo.

Mwisho japo si kwa umuhimu.

Usiseme: Somo katika ……….
Badala yake sema:Somo la …...
Usiseme: Hili ndilo neno la Mungu.”
Badala yake sema:Neno la Bwana.

Vile vile ni muhimu sana kuzingatia maelekezo unayopewa na viongozi wa liturjia mahalia.


   Tumsifu Yesu Kristo...

Post a Comment

Previous Post Next Post