HISTORIA YA MAISHA
Alfonso Maria wa Liguori alizaliwa katika familia tajiri akiwa mtoto wa kwanza kati ya wanane. Baba yake alimpatia walimu bora hivyo alivyofikisha miaka 12 alijiunga na chuo kikuu cha Napoli na kupata udaktari wa sheria za nchi na za kanisa.
Uwalimu bora ulimuingiza katika ujuzi wa biblia, historia ya kanisa na maisha ya kiroho na kujipatia elimu pana ya teolojia aliyozitumia baadae katika uandishi. Alikua pia mchoraji, mwanashauri na mwanamziki( alitunga nyimbo ya “Tu scendi dalle stelle” wa Noeli)
MAISHA YAKE YA UTAWA NA UTAKATIFU
Alijiunga seminari mwaka 1723 na kupata upadrisho tarehe 17/12/1726 akiwa na miaka 30. Alijiunga na chama cha kijimbo misheni za kitume akiwa bado kwa wazazi wake.
Mwaka 1732 alianzisha shirika lake lenye lengo la kuinjilisha maskini walioshi mashambani likakubaliwa na Papa Benedikto XIV mwaka 1749. Akapewa uaskofu wa jimbo la Sant’Agata de’ Goti mwaka 1762.
Alionesha miujiza mbalimbali ikiwemo alionekana akielea hewani mnamo 30/11/1735 kule Foggia mbele ya umati uliokusanyika mbele ya kanisa. Pia alionekana mahali pawili wakati mmoja pale Roma na katika jimbo lake mnamo mwaka 1774.
Mwaka 1775 aliacha uongozi sababu za kiafya na kuhamia kwenye nyumba ya shirika. Huko ndipo alipofariki mnamo tarehe 1/8/1787.
MTAKATIFU ALFONSO MARIA WA LIGUORI,
UTUOMBEE
إرسال تعليق