MT. YOHANE MARIA VIANNEY MSIMAMIZI WA MAPOROKO DUNIANI.
Mt. Yohane Maria Vianney alizaliwa tarehe 8/5/1786 kutoka kwenye utaifa wa ufaransa. Ni mfano bora wa kuigwa na mapadri wote duniani katika wema, upendo, ukarimu, sadaka na majitoleo yake kwa ajili ya huduma kwa watu wa Mungu.
HISTORIA YA MAISHA YA UTAWA NA UTAKATIFU.
Baada ya masomo yake ya kikasisi kwa shida kubwa alipewa Daraja takatifu ya upadre tarehe 12/8/1815. Kwa miaka 40 alijisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kuwahidumia watu wake kwa neno na sakramenti za kanisa, akajitakatifuza kwa neno la Mungu, sala, toba na wongofu wa ndani, uliofumbatwa katika maisha adili na unyenyekevu mkuu. Alijitahidi kuwaongoza watu wa Mungu katika hija ya maisha, kuelekea kwenye utakatifu na furaha ya maisha na uzima wa milele.
Alitangazwa Mwenyeheri na Papa Pio X mnamo tarehe 8/01/1905 na alitangazwa Mtakatifu na Papa Pio XI mnamo tarehe 31/5/1925. Na mnamo mwaka 1929 alitangazwa kama msimamizi wa maparoko duniani.
Alifariki tarehe 4/8/1859 akiwa na umri wa miaka 73 na miaka 40 akiwa anahudumia watu katika kumjua na kuwaweka karibu na Mungu.
MT.YOHANE MARIA VIANNEY,
UTUOMBEE.
إرسال تعليق