MT. NICODEMO MDHAMINI WA WENYE KUTAKA KUJUA.
Nicodemus alikua ni mfarisayo aliyezaliwa galilaya, mkuu wa wayahudi. Pia alikua miongoni ya wazee kwenye baraza la wayahudi. Alionekana mara tatu katika injili ya Yohana akiwa kama mfarisayo mwenye kutaka kujua zaidi kuhusu mambo mbalimbali kuhusu ufalme wa mbingu.
Yn.3; Alionekana kumhoji Yesu huku akiwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu ufalme wa mbingu.
Yn. 7:51; Alionekana kuuliza kuhusu sheria zao zinaruhusu kumuhukumu mtu kabla ya kumsikiliza wakati wakitaka kumuhukumu Yesu.
Yn.19:39; Alionekana kumsaidia Yusufu wa Arimathea kwenye kuuzika mwili wa Yesu baada ya kupewa ruhusa kuushusha na kuzika maiti ya Yesu baada ya mateso na kufa msalabani.
Hivyo hujulikana kama mdhamini kwa wale wenye uchu ya kutaka kujua mambo. Alifariki huko Judea.
MTAKATIFU NICODEMO,
UTUOMBEE
إرسال تعليق