MT. PASIFIKO DIVINI WA SAN SEVERINO
Alikuwa mtawa wa Shirika la ndugu wadogo tawi la wareformati na padri wa Kanisa Katoliki.
MAISHA YAKE MPAKA UTAKATIFU
Alizaliwa na Antonio Maria Divini na Mariangela Bruni huko San Severino, Italia tarehe 1/3/1653. Wazazi wake walifariki akiwa na umri wa miaka 3 kwa sababu ya umri mdogo alipata shida na taabu nyingi mpaka Disemba 1670 alipovikwa kanzu ya Kifransisko huko Furano.
Alipata upadrisho tarehe 4/6/1678 na kuwa mwalimu wa falsafa miaka 1680-1683. Baada ya hapo alivumilia kishujaa mateso mengi kama uwete, upofu na uziwi kwa muda wa miaka 29. Licha ya mateso hayo alikazana na maisha ya sala, akijawa na Mungu njozi na uwezo wa kutenda miujiza.
Miaka 1692-1693 alikua mhudumu wa konventi huko San Severino hadi umauti ulipomfika tarehe 24/9/1721. Kanisa humsherehekea na kumkumbuka tarehe 24/9.
MT. PASIFIKO DIVINI WA SAN SEVERINO,
UTUOMBEE.
إرسال تعليق