Somo la Kwanza
Hek 2:1, 12-22
Wasiomsadikia Mungu walisema hivi, huku
wakimfikiri yasiyo kweli, Zaidi ya hayo na tumwotee mtu wa haki, maana hatuna
haja naye, naye yu kinyume cha matendo yetu; atukaripia ya kama tumeiasi
torati, na kutushitaki ya kama tumekosa adabu. Asema ya kwamba anamjua Mungu,
na kujiita mtumishi wa Bwana. Ametuwia magombezi ya fikira zetu. Hata kumtazama
twaona ni kugumu; maan amaisha yake si sawasawa na masiha ya wengine, na
mwenendo wake ni wa kigeni. Tuanhesabiwa naye kuwa kama madini hafifu;
anajitenga na njia zetu kama na uchafu. Wenye haki asema kuwa mwisho wao ni
heri; hujivuna ya kwamba Mungu ndiye baba yake. Haya na tuone kama maneno yake
ni kweli; tufanye kujaribu yatakayompata wakati wa mwisho wake; mradi mwenye
haki akiwa ni mwana wa Mungu, Yeye atamtegemeza na kumwokoa mikononi mwa adui
zake. Na tumhakikishe kwa jeuri na maumivu, ili tujifunze upole wake na
kuithibitisha saburi yake akidhulumiwa. Hata tumhukumu auawe mauti ya aibu,
maana ataangaliwa sawasawa na maneno yake. Ndivyo walivyosemezana, wakakosea
kabisa. Kwa maana uovu wao uliwapofusha; hawakuzijua siri za Mungu; wala
hawakuutarajia mshahara wa utakatifu, wala kudhani ya kwamba iko thawabu kwao
wenye roho zisizo na hatia.
Neno la
Bwana, tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 34:16-20, 22
Uso wa Bwan ani juu ya watenda mabaya,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
Walilia, naye Bwan akasikia,
Akawaponya na taabu zao zoe.
(K) Bwana yu
karibu nao waliovunjika moyo.
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini Bwana humponya nayo yote.
(K) Bwana yu
karibu nao waliovunjika moyo.
Huihifadhi mifupa yake yote,
Haukuvunjika hata mmoja.
Bwana huzikombo a nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.
(K) Bwana yu
karibu nao waliovunjika moyo.
Shangilio
Lk 8:15
Heri wale walishikao neno la Mungu katika
moyo wao mwema na mnyofu, na wazaao matunda katika uvumilivu.
Somo la Injili
Yn 7:1-2, 25-30
Baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika
Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuw
awakitafuta kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye
laipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. Basi baadhi ya watu wa
yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? Na kumbe! Anena
waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu tuna jua hakika ya kuwa huyu
ndiye Kristo? Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna
ajuaye atokako. Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema,
Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye
aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka
kwake, naye ndiye aliyenituma. Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu
aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.
Neno la
Bwana, Sifa kwako ee Kristo.
إرسال تعليق