![]() |
Historia yake.
Sikukuu ya Bikira Maria Malkia ilipewa nafasi katika Liturujia ya Kanisa miaka mingi iliyopita mnamo mwaka 1955 Papa Pius wa kumi na mbili alipoandika katika orodha ya maadhimisho rasmi.
Hata hivyo jina la Malkia ni moja wapo ya majina ambayo Kanisa limeyatumia tangu zamani kwa kumheshimu Mama wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Sala ya Malkia wa Mbingu, furahi, aleluya, ambayo husaliwa badala ya Malkia wa Bwana katika Kipindi Cha Pasaka ni Sala ya zamani sana.
Siku hizi Kanisa katika Sala yake rasmi ya asubuhi husalilisha hivi Kristo Mfalme alimtawaza Mama yake awe Malkia wa Mbingu.
Sikukuu hii ilipoadhimishwa kwanza katika Liturujia ya Kanisa, siku yake yenyewe ilikuwa tarehe 31 mwezi wa Tano ulio kuwa mwezi wa Maria hasa.
Lakini badaye tarehe yake ikawa 22 mwezi Agosti yaani juma Moja baada ya Sherehe ya kupalizwa kwake Mbinguni mwili na Roho ili kuonesha wazi uhusiono uliopo kati ya Sherehe hiyo na hadhi yake ya ki Malkia.
Hasa kwa sababu amepalizwa hivyo Maria anaweza kukamilisha Mchango katika kazi ya wokovu ya mwanae Yesu.
Ieleweke vema kamba, Maria ni Malkia wa Mbinguni yeye ni Malkia wa Mababu wa Mitume wa Mabikira na wengine, vilevile Maria ni Malkia wetu sisi Wanadamu na hata Malkia wa Ulimwenguni wote.
Huduma zile alizozitoa hapa duniani zamani zile Nyumbani mwa Ndugu Elizabethi, Nyumbani mwana mumewe Yosefu ambaye Pamoja naye alimtunza mtoto Yesu kule Nazareth, kule Kana siku ya harusi divai ilipoisha, na zaidi ya yote, alipokuwa amesimama karibu na Msalaba wa Yesu huduma zake hizo hazijakoma.
Sasa akiwamo Mbinguni akiwa Malkia wa Mbingu na duniani, akiwa na Mama yetu Maria Mama wa Kanisa akiendelea na kutulinda kwa Upendo wake wa kimama, watu wote wapate kumfikia ukweli halisi na kushiriki Wokovu aliowastahili Kristo Yesu alipotezwa na kufa Msalabani.
Utunzaji wake wa kimama unaendelea kabisa, nasi wanae hatuna budi kumwitiakia kwa dhati tusikiapo maneno aliye waambia zamani watumishi kule Kana, fanyeni yote Yesu atakayo waambia, kumwitiakia huko ndiko ishara ya wazi ya kumheshimu na kumpenda Mama Maria Malkia wetu kwa namna hiyo twadhihirisha wazi kwamba Maria anayo Maana Kweli Katika Maisha yetu ya kila siku.
BIKIRA MARIA MALKIA WA MBINGU, UTUOMBEE.
إرسال تعليق