MTAKATIFU BERNARD, ABATE NA MWALIMU WA KANISA

Kanisa linafanya kumbukumbu kwa heshima ya Mtakatifu Bernard aliyezaliwa mwaka1090 huko Fountaine-les-Dijon nchini Ufaransa. Alizaliwa katika familia iliyoheshimika sana.

Alisoma pia katika shule bora na alipenda pia masomo ya Biblia. Mwaka 1111 Mtakatifu Bernard na vijana wengine 30 walijiunga na Monasteri ya Citeaux ambayo ilikuwa chini ya Wabenedictine. 

Mnamo waka 1115  Mtakatifu Bernard na wenzake 12 walienda kuanzisha monasteri mpya ya Clairvaux. Naye akachaguliwa kuwa Abate na katika kipindi kifupi walipokea vijana 130 ambao walijiunga nao . Mtakatifu Bernard alikuwa karibu na Askofu William wa Champeaux.

Kutokana na wingi wa watawa mwaka 1118 Mtakatifu Bernard alituma Watawa kwenda kuanzisha monasteri huko Chalons.

Kutokana na busara na hekima zake Mtakatifu Bernard alitumika kutatua matatizo katika kanisa katika ngazi zote.Alipata muda pia wa kuandika nyaraka mbalimbali aliwaelewesha na kuwafundisha pia wapinga Kristo.

Mtakatifu Bernard aliendelea pia na uinjilishaji akatuma Watawa katika nchi mbalimbali za Ulaya. Mtakatifu Bernard alikufa  August 20, 1153 huko Clairvaux katika Taifa la Ufaransa.

Alitangazwa Mtakatifu Januari 18, 1174 na Baba Mtakatifu  Alexander III. Mtakatifu Bernard alitangazwa kuwa Mwalimu wa Kanisa mnamo mwaka 1830.

 

Pia Watakatifu wafuatao wanakumbukwa kwa tarehe ya leo ambao ni pamoja na:

Mt. Amadour

Mt. Baamin

Mt. Bernard wa Valdeiglesias

Mt. Edbert

Mt. Haduin

Mt. Heliodorus

Mt. Herbert Hoscam

Wt. Leovigild na Christopher

Mt. Lucius

Mashahidi wa Thrace

Mt. Maximus

Mt. Philibert

Mt. Ronald

 

Mtakatifu Bernard, Wakatifu na Wenyeheri mtuombee kwa MUNGU ili tustahili neema ya utakaso katika maisha yetu.

Post a Comment

أحدث أقدم