
Monika alizaliwa mwaka 331 huko Tagaste (Algeria)
Tangu utoto wake alifundishwa kumtumikia Mungu na kujitenga na dhambi.
Monika alizoea kwenda kusali peke yake Kanisani alikuwa akiwapenda maskini na aliwagawia chakula chake.
Alipokuwa Wazazi wake wakamuozesha kwa kijana mmoja jina lake Patriki, ambaye alikuwa mtu wa ukoo bora lakini hakuwa Mkristo na alikuwa mwepesi wa kukasirika .
Monika alistahimili kwa upole alipogombezwa na mumewe alizaa watoto watatu na mmoja wao ndiye Augustino, Mwalimu wa Kanisa.
Monika aliwalea wanawe katika dini ya kweli wakiwa wadogo bado aliwafundisha kumpenda Bwana wetu Yesu Kristo na kulitaja jina lake kwa heshima hata Mume wake Patriki naye akaongoka akawa Mkristo kwa sababu ya mwenendo safi wa Monika.
Augustino mwanawe alienda kukaa Kartago (Tunisia) ili asome shule, akaendelea katika maarifa yote lakini alizidi kufanya uasherati na mambo yote yasiyofaa.
Alimsikitisha sana mama yake, Monika alimwendea Askofu mmoja wa huko akamuliza “Itakuwaje na mwanangu?”.
Naye Askofu akamjibu Usiogope mama mtoto huyu wa machozi mengi hivi hawezi kupotea kweli Monika hakumuomba Mungu bure maana Augustino aliongoka akabatizwa na Mtakatifu Ambrosi (7 Desemba) akawa mwalimu shujaa wa mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Monika alipojiona karibu kufa, aliwaambia wanawe. ‘Mnizike mpendavyo ila nawaombeni kitu kimoja Mnikumbuke kwenye altare ya Bwana.'
Akafa huko Ostia (Italia) mwaka 387.
MTAKATIFU MONIKA, UTOMBEE..
إرسال تعليق