Mtakatifu Pius wa Kumi, Papa(1914)

Pius wa Kumi aliyeitwa Yosefu Sarto kabla ya kuwa Papa, alizaliwa Riese katika mkoa wa Venisi (Italia) mwaka 1835. 

Wazazi wake hawakuwa wa asili bora lakini walikuwa watu wa mwenendo mzuri na wachaji wa Mungu.

Alipata Upadre na akafanya vizuri sana kazi kama Padre msaidizi baadaye kama Paroko na kiongozi wa mambo ya kiroho katika Seminari ya Jimbo lake.

Baada ya kuwa kwanza Askofu wa Mantua na halafu Askofu Mkuu

wa Venisi aliteuliwa kuwa Papa mwaka 1903.

Alipochaguliwa kuwa Papa, alikataa kwa kulia machozi lakini hata hivyo kulia kwake kulikuwa kazi bure.

Kisha kuonywa akaupokea huo mzigo kwa maneno haya: "Naupokea kama msalaba".

Kweli aliupokea utawala huu mkuu kama msalaba alioupatakwa Mwenyezi.

Hakuyaacha maisha yake ya zamani akaendelea na unyofu hivi kwamba aliweza kuandika bila uwongo, karibu na mwisho wa maisha yake, kama hivi: "Nilizaliwa maskini, nikaishi maskini, napenda kufa maskini".

Aliliongoza Kanisa kwa uthabiti katika misukosuko ya mwanzo wa karne ya ishirini. 

Msimamo wake ulikuwa kuviweka tena vitu vyote chini ya Kristu. 

Alianzisha vyama vizuri vya kila aina; muziki wa Kanisa ukarudishwa katika uzuri na utukufu wake kama zamani akaanzisha mafunzo ya Biblia huko Roma akatengeneza kwa ustadi mkuu lile Baraza Kuu la Kanisa la Roma. 

Pia alitengeneza mipango yą kuwafundisha waumini katekismu akaingiza desturi ya kupokea komunyo mara nyingi zaidi, hata kila siku akakubali watoto wadogo wanapopata akili, wapokee komunyo.

Kwa jitahada kubwa aliweka msingi wa Utume wa Walei

Wakatoliki kulingana na mpango rasmi na wakati ule, utume huo uliitwa Aksyo Katoliki maana yake utendaji wa Kikatoliki.

Alijishughulisha kutengeneza maisha ya kitawa na akaongeza seminari katika nchi mbalimbali. 

Aliwahimiza Mapadre wote waishi maisha mazuri ya kiroho. 

Sheria za Kanisa zilifanywa ziwe na nia moja tu. Alilaumu na kuonyesha waziwazi potovu zote za hatari katika kueleza Biblia na mambo makuu ya dini ya kikatoliki ziitwazo "mnodernism" yaani "mambo leo".

Akakataa na kutupilia mbali ile haki ya serikali kuwa na usemi katika uchaguzi wa Papa.

Mwishowe kwa ajili ya kuelemewa na kazi ngumu, na kudhoofika kwa huzuni kubwa kwa ajili ya vita vilivyoanza siku zile Ulaya, akaaga dunia 20 Agosti 1914. 

Kiisha kufanyika miujiza kwa maombezi yake akatajwa Mtakatifu mwaka 1954 kwa shangwe kubwa.


MTAKATIFU PIUS WA KUMI PAPA, UTUOMBEE..

Post a Comment

أحدث أقدم