
MAISHA YA MTAKATIFU GREGORI MKUU (6O4) PAPA NA MWALIMU WA KANISA.
Gregori alizaliwa Roma (Italia) mwaka 540.
Kwanza alikuwa mtumishi wa serikali alipewa wadhifa wa kuwa kadhi wa Roma.
Kisha alipofiwa na baba yake alitumia urithi wake kwa kujenga Monasteri moja Roma na Monasteri sita kisiwani sisilia.
Alipokuwa na umri wa miaka Thelathini na mitano aligeuza nyumba yake iwe Monasteri na yeye mwenywe akawa Mmonaki akapewa Ushemasi halafu alipelekwa kama Balozi wa Papa Konstantinopoli (Uturuki) akakaa huko muda ya miaka sita.
Baadaye alirudi kwenywe Monasteri yake mjini Roma (Italia).
Tarehe 3 Septemba 590 aliteuliwa kuwa Papa ndiyo mtawa wa kwanza kuchaguliwa kuwa Papa.
Katika mambo makuu aliyotenda Mtakatifu Gregori yanayosifiwa hasa ni Kubatizwa kwa Walombaridi ( Italia ya Kaskazini) na kuwahubiria dini Katoliki waingereza.
Kuna hadithi isemayo kwamba siku moja akiwa mmonaki, alipokuwa akitembea mjini Roma akafika sokoni walipokuwa wakiwekwa watumwa wa kuuzwa.
Gregori alipendezwa na vijana hao akauliza walikotoka wakamwambia kuwa wao walikuwa Waingereza alafu haifai watu wazuri namna hii wawe watumwa wa shetani mara akaenda kwa Papa saa ile ile akamwomba awapeleke Mapadre huko Uingereza wapate kuwaongoa watu wa huko.
Akaomba pia yeye mwenyewe awe mmoja wao Papa akakubali, lakini baada ya muda kidogo aliambiwa kurudi Roma kwani watu wa pale walitaka abaki kwao tu yeye mwenywe alipochaguliwa kuwa Papa bila kukawia alipeleka Wamisionari arobaini kueneza neno la Mungu huko Uingereza.
Mtakatifu Augustino wa Kanterbury alikuwa ndiye mkubwa wao, Papa Gregori alijitahidi sana kutunga muziki kwa ajili ya adhimisho zuri la Ibada za Liturujia na hivyo alivumbua namna ya kuandika mpangilio wa noti uitwao muziki wa kigregori aidha alikuwa mnyenyekevu sana.
Katika barua zake alizoea kujiita Mtumishi wa Watumishi wa Mungu na tangu hapa mpaka hivi leo Mapapa wote hujiita hivyo.
Kazi yake katika kuieneza na kuimarisha imani ya Kikristo inadhihirisha ya kwamba yeye alikuwa mchungaji wa kweli isitoshe ameandika mambo mengi kuhusu imani na maadili bora ya Kikristo.
Alikufa mwaka 604.
MTAKATIFU GREGORY MKUU PAPA NA MWALIMU WA KANISA, UTUOMBEE..
إرسال تعليق