MAISHA YA MTAKATIFU ROSALIA WA PALERMO
Mtakatifu Rosalia anaheshimiwa sana kisiwani Sisilia (Karibu na Italia) alipozaliwa na Wazazi wa jamaa bora.
Alipopata umri wa makamu aliacha anasa za dunia walizozoea kukimbilia vijana wanawake.
Akaenda kukaa pangoni karibu na Palermo mle pangoni huonekana altare aliyoichimbwa maweni.
Baadaye alihamia mahali pa upweke mlimani Peligrina.
Huko ndiko alikokaa mpaka kufa kwake akisali na kufanya kitubio.
Miujiza mingi imetendeka kwa maombezi ya Mtakatifu Rosalia na mapango yote mawili yametengenezwa kuwa Kanisa watu wengi huenda kusali humo.
MTAKATIFU ROSALIA WA PALERMO, UTUOMBEE..
إرسال تعليق