MAISHA YA MWENYEHERI YOHANI GABRIEL PERBWAYE MFIADINI (1840)

Yohani Gabrieli Perbwaye ( Perboyer) alizaliwa Ufaransa na Wazazi Wakristo waliokuwa wakulima.

Yohani alikuwa ni mtoto wa tano kwa wazazi wake kutokana na akili yake kubwa angaliweza kujipatia ukuu mbele za watu. Furaha moyoni mwake kwa kumtumikia Mungu wakati angali mtoto bado alizoea kusema “Nitakuwa Padre mmisionari”

Alipopata umri wa miaka kumi na minane aliingia katika Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo akajifunza akapewa Upadre halafu akapanda merikebu akaenda China kuhubiri huko injili ya Yesu Kristo.

Alijitahidi kwa muda wa miaka minne kuwahubiria wachina neno la Mungu.

Mara udhalimu Kwa Wakristo ukajitokeza Makafiri walituma askari kwenda kumkamata Padre Yohani pamoja na Mapadre wengine watatu.

Mapadre waliposikia habari hii wakajificha mwituni lakini Mkristo mmoja aliwaarifu askari mahali mapadre hawa walipojificha Kama Yuda aliwatoa mikononi mwa adui zao kwa vipande thelathini vya Fedha. 

Padre Yohani alikamatwa wakamtupa gerezani wakamtesa vikali.

siku moja wakautupa msalaba chini mbele ya miguu yake wakimwambia Haya mkanyage Mungu wako, halafu tutakupa ruhusa uende zako lakini Padre huyu akawajibu 

“Siwezi kabisa kumkanyaga Mungu wangu”

Aliokota Msalaba akaubusu kwa heshima Mara askari wakampiga fimbo mara mia akahukumiwa auawe kwa kunyongwa halafu wakamrudisha gerezani na humo alishinda bado miezi sita akiwashangaza wachina kwa uvumilivu wake.

Aliilainisha mioyo ya walinzi wake, ambao waliwapa ruhusa Wakristo waingie na kumwangalia ndivyo Padre alivyoweza kupokea Sakramenti akiletewa Ekaristi na Padre Mchina.

Mwaka 1840 tarehe 11 Septemba siku ya ijumaa yapata saa tisa hivi alipelekwa kunyongwa na hiyo ndiyo iliyokuwa saa Mwokozi alipokufa msalabani hapo zamani. 

Papa alimtaja kuwa Mwenyeheri mwaka 1889.

MWENYEHERI YOHANI GABRIELI PERBWAYE MFIADINI, UTUOMBEE..

Post a Comment

أحدث أقدم