MAISHA YAO

Watakatifu mashahidi wafiadini Kosma na Damiano tunaowakumbuka leo walikuwa ndugu mapacha waliozaliwa huko Arabia miaka ya mwanzo ya Ukristo. walisoma na kufudhu vizuri katika tiba na sayansi ya madawa. Tangu utoto wao Cosmas na Damiano walijawa na moyo wa upendo na kuwahudumia watu.

kama wakristo, walitumia taaluma yao kuwahudumia wagonjwa. kama matatibu walipata fursa za kuingia katika nyumba za wapagani kutoa huduma. Walipendwa sana na watu wote kwani kamwe hawakuchukua fedha kwa huduma walizozitoa, hivyo watu waliwaita “Watakatifu bila fedha”

Muujiza wa Kosma na Damiano. Inasemekana walimponya mtu aliyepata shida ya mguu. kwa msaada wa Mungu walimbadilishia mkuu mtu mweupe aliyekuwa mgonjwa kwa kumwekea mguu wa mtu mweusi wa Ethiopia aliyekuwa amekufa karibuni.

wakati wa madhurumu ya Diokletiani, Watakatifu Kosma na Damiano waliteswa vikali na hatimaye kuuawa kwa sababu ya imani yao. Watakatifu Kosma na Damiano ni wasimamizi na waombezi wa Wafamasia.

tunapowaenzi hawa, tumuombe Mungu atujalie kuwahudumia wenzetu bila kujali faida, tukikumbuka maneno ‘tenda wema na uende zako’ na maneno ya Kristo katika Injili “Sisi ni watumishi tusio na faida tumefanya tu yale yatupasayo”

watakatifu Kosma na Damiano mashahidi mtuombee..

Post a Comment

أحدث أقدم