LEO OKTOBA 13, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU EDWARD, MWUNGAMA DINI (1066)

Edward alikuwa mwana wa Etelredi Mfalme wa Uingereza, tangu Utoto wake Edward alisifiwa sana hivi kwamba watu walimwita Malkia wa Ikulu.

Zamani hizo watu wa Denmark walishambulia Uingereza na Edward ilimpasa kukimbilia kwa mjomba wake aliyekuwa akikaa Normandia (Ufaransa).

Majambazi wa Denmark wakaiteka Nchi, baadae Edward alirudi Uingereza akashangiliwa kwa furaha Kuu.

Muda si muda akaanza kuzijenga upya Kanisa zilizobomoka. 

Alitunga sheria nzuri za kutawala nchi na muda kidogo mambo yote yalitengemaa na Nchi ikarudia amani kama zamani.

Kwa kushauriwa na wazee wa Nchi. 

Aliona kijana mwanamke mzuri jina lake Edita. Hawakudiriki kupata watoto. 

Mtakatifu Edward alikuwa mkarimu sana kwa wagonjwa na masikini, jambo la kutoa kwa masikini lilimfurahisha sana, pia alijengesha Monasteri kubwa kule Westminster. 

Alifariki mwaka 1066, Juma moja tu baada ya Monasteri hiyo kuzinduliwa, akazikwa humo humo nyuma ya Altare Kuu ya Kanisa la Monasteri .

Yeye huitwa Mtakatifu Edward Mwungama Dini kwa kuwa maisha yake yote yalikiwa mfululizo wa matendo ya kumshuhudia Kristo.


MTAKATIFU EDWARD, MWUNGAMA DINI, UTUOMBEE..

Post a Comment

Previous Post Next Post