BIKIRA MARIA MAMA YETU WA ROZARI
Rozari ni Sala, ama tungo la Sala ya Baba yetu' na Sala ya ' Atukuzwe Baba .... ' husaliwa mara kumi na tano kila moja na Ile Sala ya maamkio ya Malaika husaliwa mara mia Moja na hamsini.
Kwa Sala hiyo, Waamini hufundishwa jinsi ya kumheshimu Mkombozi wetu kwa kuyawaza Matendo makuu kumi na matano ya Maisha yake na Mama yake.
Kwa hiyo, Rozari ni Injili kwa Ufupi, historia ya maisha ya Yesu Kristo. Katika Ibada hii ya Rozari, Lengo kubwa kwa Waamini sharti daima liwe katika kuyatafakari Matendo haya; Kumrudishia Mungu Shukrani kutokana na Matendo haya.
Matendo haya ya Rozari yanatakiwa kuwa ni Kipindi cha muumini kuimarisha mwenendo wa maisha kadiri yanavyo vuta Moyo wake.
Sala ya Rozari ni rahisi kusalika na kila mtu, zaidi ya hayo ni Sala iliyo maarufu sana.
Mwaka 1572, Papa aliwamuru Waamini waitukuze kila mwaka, Sikukuu ya Bikira Maria Mama Yetu Mshindi, Ili kumwomba Mungu huruma yake kwa Kanisa na kwa ajili ya Waamini wote, na kumshukuru kwa Ulinzi wake hasa kwa kuliokoa Kanisa kutoka katika mikono ya Waturuki Waislamu waliotaka kuliangamiza.
Ushindi huo, katika Vita vya baharini vilivyopiganwa huko Lepanto ( Ugiriki) ulionekana kuwa umepatikana kutokana na sala na mandamano ya vyama vya Rozari mjini Roma, yaliyo Fanya Wakati wa Mapigano hayo ya Lepanto.
Kumbukumbu hii inawakumbusha Waamini wote kufanya fikara juu ya mafumbo ya Kristo, kwa kufuata mfano wa Bikira Maria, ambaye kwa namna ya pekee alihusika na kuzaliwa, kuteswa na kufufuka kwa Mwana wa Mungu.
BIKIRA MARIA MALKIA WA ROZARI TAKATIFU, UTUOMBEE..
Post a Comment