Somo la Kwanza
Rum
12:5-16
Sisi
tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa;
ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani; ikiwa huduma, tuwemo katika
huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo
mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidi; mwenye kurehemu, kwa furaha.Pendo na lisiwe
na unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la
udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii,
si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini,
mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya
watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.
Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio;
lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu,
lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.
Neno la Bwana, Tumshukuru Mungu.
Wimbo
wa Katikati
Zab
131
Bwana,
moyo wangu hauna kiburi,
Wala
macho yangu hayainuki.
Wala
sijishughulishi na mambo makuu,
Wala
na mambo yashindayo nguvu zangu.
(K) Moyo wangu uwe na
Amani kwako, Ee Bwana.
Hakika
nimeituliza nafsi yangu,
Na
kuinyamazisha.
Kama
mtoto aliyeachishwa
Kifuani
mwa mama yake;
Ndivyo
roho yangu ilivyo kwangu.
(K) Moyo wangu uwe na
Amani kwako, Ee Bwana.
Ee
Israeli, umtarajie Bwana,
Tangu
leo n ahata milele.
(K) Moyo wangu uwe na
Amani kwako, Ee Bwana.
Shangilio
Zab
147:12,15
Aleluya, aleluya,
Msifu
Bwana, Ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
Somo
la Injili
Lk
14:15-24
Mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu. Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi, akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya miji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, n ahata sasa ingaliko nafasi.Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Neno la Bwana, Sifa kwako Ee Yesu Kristo.

Post a Comment