MUNGU kupitia Kanisa lake takatifu ulimwenguni mwote huweza kuwaunganisha mke na mume kuwa mwili mmoja kupitia sakramenti ya ndoa takatifu.Sakramenti ya ndoa takatifu huhimiza Zaidi na kusisitiza waumini kuishi Katika ndoa zilizo Katika misingi ya ukristo.Hivyo tuangalie juu Zaidi ya maana ya ndoa ya kikristo.
MPANGO NA SIFA YA NDOA YA KIKRISTO.
Sasa tuchungulie juu ya ndoa ya kikristo na mpango wake.Kanisa linafuata matendo na maneno ya Mungu Katika mpango wa ndoa yake.
NI MUNGU ALIYEWEKA NDOA.
Umesikia ya kwamba ni Mungu aliyeiweka ndoa paradisini.Adamu alipoumbwa aliona furaha na heri.Lakini baada ya siku si nyingi alianza kuona ukiwa.Akaenda kumtafuta mwenzake apate kuongea naye,asimwone;aliwatazama wanyama wote akitumaini mmojawapo ataweza kuwa mwenzake ,lakini alishindwa kumkuta mwenzake afaaye.Katika shida hiyo Mungu alimwonea huruma.Alimtia usingizi mzito,akaumba mtu wa pili kwa ubavu wa Adamu.Naye alikuwa mtu kama Adamu lakini mke.Mara Adamu aliona;Huyu ni mwenzangu kwelikweli ;naweza kuongea nae vizuri,ananifahamu.Teana ana majaliwa ninayokosa mimi,hasa maoni ya moyo.Basi,Napata faida kwake.Kadhalika na Eva aliona :Mtu huyu ananifaa,ana akili nyingi na nguvu kuliko mimi. Kwake Napata ulinzi na msaada.
Hivyo kila mmojawapo aliongezeka Katika hali yake kwa majaliwa ya mwenzake ,yaani walitimizana. Zaidi ya hayo walipendana sana,maana mke alimwelekea mume aliyekuwa asili yake ,na mume alimwelekea mke aliyekuwa kwanza sehemu ya mwili wake mwenyewe.Tabia hiyo ya kuelekeana mwanaume na mwanamke imeithiwa na mwenzake wa ndoa roho kwa roho,moyo kwa moyo.Basi ,kwanza Mungu alituliza hamu ya mwanadamu apendane na mwenzake wa ndoa roho kwa roho,moyo kwa moyo.
NI YESU ALIYEIKUZA NDOA.
Yesu alipofundisha duniani alithibitisha mpango huo wa ndoa,yani mapendo kati ya mke na mumwewe yawe msingi wake.Tena ameinua ndoa na kuiweka Katika daraja la sakramenti.Sakramenti hiyo inawatakasia watu wa ndoa mapendo yale yaliyowavuta waoane.Kwa hiyo hawapendi kwa mapendo ya kibinadamu tu,wanazidi kupendana kwa mapendo matakatifu ya Mungu yaliyoongezwa Katika kupokea sakramenti ya ndoa.
Mtume Paulo ameandika : “Enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo alivyolipenda kanisa lake akajitoa kwa ajili yake….”(Waefeso 5:25).Lakini Kristo ameungana na kanisa lake kwa njia ya kiroho.Hivyo watu wa kanisa waungane hasa roho kwa roho,moyo kwa moyo. Wakiungana na kupendana hivyo katia roho zao na kutiwa sahihi ya Mungu Katika sakramenti ,ndoa yao ni kweli takatifu,tena nzuri na safi.
MAHUSIANO YA ROHO NI MUHIMU TENA YA KWANZA.
Baba mtakatifu Pio wa XI ameandika hivi: “Katika ndoa mume na mke wanaungana kuwa umoja Katika roho,tena kabla ya kuungana Katika mwili. na Zaidi kuliko mwilini.Wala hawaungani tu kwa tamaa inayopita ,tena au kwa mvuto wa moyo tu,bali kwa kutaka kabisa kwa akili na kwa niathabiti,Basi ndoa takatifu isiyofunguka ina asili na msingi wake Katika maungano hayo ya roho.Hivyo imetakiwa na Mungu .Ndoa hiyo ni tofauti na maungano ya wanyama wasio na akili ,wanaofuata silika tu bila kufahamu na hiari;tena ni tofauti na maungano ya ovyo ya wanadamu wasiotegemea maungano ya kweli ya utashi wao kwa kadiri ya sheria.”
INA NIA YA KUPATA WATOTO.
Baada ya kuwatimizia watu wa kwanza hamu yao ya kupendana na kusaidiana ,Mungu aliwaambia : “Mzidi mkaongezeke…”.Kwa maneno hayo Mungu amewapa watu ruhusa kuzaana watoto.Mapendano yao Katika mwili ni nyongeza tu nay ale mapendano ya roho ,tena yanakuzwa na kutakaswa na mahusiano ya roho.Juu ya hayo ni Mungu aliyempa mume uwezo wa ubaba na mke uwezo wa umama.Hivo washirikiane nae Katika kuumba.Kwa kuwa kuzaa watoto nk tendo takatifu ,Mungu ameiweka sharia ya kutumia uwezo wa kuzaa Katika ndoo tu.Tena Yesu kristo ametufundusha namna ya kuingia ndoa,yaani kwa mlango wa skramenti .Watu wasikutane tu kama wanyama ,bali wafunge mapatano matakatifu mbele ya Mungu ,na kwa baraka yake wapendane na kutimiza mambo ya ndoa.
Mpaka sasa tumeona :Ndoa ni mapendano ya roho kati ya mwanmamume mmoja na mwanamke mmoja kwa nia ya kuzaa watoto ,imekuzwa na Kristo na kupewa cheo cha sakramenti,inadumu mpaka kufa mme au mke.
MKE NI CHINI YA MUME WAKE ,LAKINI NI MWENZI WAKE
Katika kila jumuiya sharti mmoja awe mkubwa .Kama wote ni sawa na kila mmoja aweza kufanya apendavyo ,jumuiya hiyo haiwezi kudumu ,maana itafanya fujo tu .Vivyo hivyo watu hawawezi kufanikiwa hata Katika jumuiya ndogo kama ndoa na familia pasipo mkubwa .Sharti mmoja awe mkubwa.
Katika hayo ndoa ya kikristo inafuatia pia mpango uliowekwa na Mungu.Dhambi ya asili haikuweza kuharibu mapendano yaliyoko kati ya mume na mke ,lakini imepunguza mapendo hayo.Mungu alipotangaza hukumu kwa kila mmoja baada ya kutenda dhambi alimwambia mwanamke "hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako;kwa utungu utazaa watoto;na tamaayako itakuwa kwa mumeo ,naye atakutawala"(Mwanzo 3:16). Neno hii “naye atakutawala ” laonyesha ya kuwa mkubwa Katika ndoa ni mume .Basi dini ya kikristo yataka hii :mume awe mkubwa Katika ndoa ,lakini amsimamie mke wake kwa mapendo ya moyo.Naye mke amnyenyekee mume wake kwa upendo,afurahi aweze kumnyenyekea kama bwana na kumfurahisha.Akifanya hivyo ,atazidi kuona heri kwa kadiri moyo wake ulivyoumbwa.
Baba Mtakatifu Pio wa XI ameeleza mahusiano hayo kwa maneno mazuri sana.Ameandika: “Familia inaunganishwa kuwa umoja kwa kifungo thabiti cha mapendo.Kwa hiyo utaratibu wa mapendo lazima upate haki yake,mume amewekwa juu ya mke na watoto ,na mke amnyenyekee mume kwa mapendo na kumtii kwa hari ,jinsi mtume Paulo alivyosema kwa maneno haya: “ Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. ”(Waefeso 5:22-23). Sheria imlazimishayo mke kwa haki , kwa kuwa ana cheo cha mwanadamu na wajibu mtakatifu,yaani kuwa mke,mama na mwenzi wake mume.Wala haimwamuru kutii matakwa yoyote ya mume hasa yasiyo na maana au kutweza cheo cha mwanamke.Wala haitaki kusema kwamba mke amewekwa Katika daraja moja na watu wanaotazamwa sheriani kama watoto wasioruhusiwa kutumia haki zao kwa hiari yao,kwa kuwa hawajakomaa bado na kukosa maarifa.Inayokataza sharia hiyo ndiyo ujuaji na uhuru kupita kiasi bila kuangalia salama ya familia.Inayokatazwa ndiyo kutenga moyo na kichwa ,kwa maana utengano huu waudhuru umoja wa famiilia,ukautia Katika hatari kubwa ya kuangamia kabisa,Kwa mana kama mume alivyo kichwa ndivyo mke alivyo moyo ;kama impasavyo mume kuongoza,ndivyo impasavyo mke ayatazame mapendo kuwa hasa mamlaka yake”(Casti Connubii)
Hapo hatuna neno la kuongeza .Uzuri wa mafundisho hayo unang'aa wenyewe.

Post a Comment