SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI  NI NINI?

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi. Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea.

Kwa mujibu wa WHO ulimwenguni kote saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya nne kwa kuathiri wanawake, ikiwa na wagonjwa wapya 604,000 mnamo 2020. Takriban asilimia 90 ya vifo 342,000 vilivyosababishwa na saratani ya shingo ya kizazi vilitokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Viwango vya juu zaidi vya saratani hiyo na vifo ni kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika ya Kati na Kusini Mashariki mwa Asia. 

Takwimu za WHO zinaonesha kuwa kila mwaka Tanzania ina wagonjwa wapya wa saratani 42,000 ambapo wagonjwa hao wapya wanaofika kwenye vituo vya afya ni takribani 15, 900 tu.  


NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI?

Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana.


BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA HATARI ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

1.Kushiriki tendo ndoa katika umri mdogo au chini ya miaka 18.

2.Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti.

3.Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system).

4.Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi.

5.Uzazi wa mara kwa mara


BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

1.Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.

2.Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa.

3.Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area).

4.Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.

5.Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia.

6.Mkojo wenye matone ya damu.


JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA?







Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema. Matibabu yanaweza kujumuisha:

1.Upasuaji

2.Mionzi

3.Tibakemikali


Saratani ya mapema ambayo bado haijasambaa nje ya uso wa seviksi yako inaweza kuondolewa kwa upasuaji. Madaktari wanahitaji kutoa kipande cha kizazi chako tu (sio seviksi au uterasi yako yote) na upasuaji hufanywa kupitia uke wako. Taratibu zinajumuisha:

LEEP—waya nyembamba inayotumiwa pamoja na umeme kuondoa saratani

Leza—utaratibu huu unaweza kufanywa ofisini kwa daktari wako kwa kutumia dawa ya kutia ganzi kwenye maeneo ya tishu isiyo ya kawaida kwanza.

Upasuaji—upasuaji huu unafanywa hospitalini ukiwa umelala

Upasuaji huu hauathiri uwezo wako wa kupata mimba. Hata hivyo, utalazimika kujifungua watoto wako kupitia Upasuaji.


Saratani iliyoendelea zaidi ambayo haijaenea sana inaweza kutibiwa kupitia histerektomia. Katika histerektomia, daktari hutoa uterasi yako na wakati mwingine tishu zilizo karibu nayo. Wakati mwingine, madaktari watafanya tiba ya mionzi baada ya histerektomia. Ikiwa saratani imeenea, madaktari wanaweza kukupa tiba ya mionzi pamoja na tibakemikali pekee. Baada ya tiba ya mionzi na tibakemikali, wakati mwingine madaktari hufanya upasuaji ili kuondoa saratani iliyobaki.


JE NI NJIA GANI HUTUMIKA KUPIMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

1.PAP test

Madaktari wanaweza kutumia kipimo cha pap kugundua saratani ya Shingo  ya kizazi  na displasia ya mlango wa kizazi (ukuaji wa seli zinazoweza kusababisha saratani) Uchunguzi wa Pap unafanywa wakati wa uchunguzi wa fupanyonga.

Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza sehemu ya ndani ya uke wako kwa kuufungua akitumia kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu.Katika uchunguzi wa Pap, daktari wako huchukua seli kidogo kutoka kwa seviksi yako kwa kutumia usufi,Seli hizo huchunguzwa kwenye hadubini

Daktari akiona kuwa seli zako zinaonekana kuwa si kawaida, atachukua kipande kidogo cha seviksi yako ili kukichunguza kwa hadubini (kuondoa kipande cha tishu kwa uchunguzi).Ikiwa una saratani ya mlango wa kizazi, madaktari wataona ukubwa wa saratani hiyo na imeenea kwa kiasi gani kwa kutumia vipimo kama vile:


2.Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)

Uchunguzi wa picha ambao huchukua eksirei kutoka pembe nyingi ili kuunda picha ya kina ya ndani ya mwili wako


3.Upigaji picha kwa mvumo wa sumaku (MRI)

Kipimo cha upigaji wa picha kinachotumia sehemu thabiti ya sumaku kuuunda picha yenye maelezo ya kina ya ndani ya mwili wako.


UMRI WA KUPATA PAP TEST

   Test hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65 na chini ya umri wa miaka 21 endapo ameingia katika tendo la ndoa kwa kipindi kisichopungua miaka 3. 


HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUPUNGUZA HATARI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

1.Pap tests.

Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo    wako wa maisha. 

2.Pata HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari) . 

Unaweza kusaidia kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa kupata chanjo ya HPV (sindano) ukiwa mdogo.Chanjo hii hutolewa kwa dozi 2 au 3, kulingana na umri wa mtoto wakati wa kupata chanjo ya kwanza.

Madaktari wanapendekeza wasichana na wavulana kupata chanjo hiyo wakiwa na umri wa miaka 11 au 12

Ikiwa hukupata chanjo ukiwa na miaka 11 au 12, unaweza kupewa na madaktari hadi ufikishe miaka 27.

Watu wazima wenye umri wa miaka 27 hadi 45 ambao hawajachanjwa wanapaswa kuzungumza na madaktari wao kuhusu iwapo wanapaswa kupewa chanjo.







3.Kuwa na mpenzi mmoja. 

Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa. 

4.Chukua tahadhari na hatua stahiki za kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa

Post a Comment

Previous Post Next Post