NOVENA KWA MTAKATIFU YOSEFU MFANYAKAZI
1. KUFUNGUA
❖ Kwa Jina la Baba, na la mwana, na la Roho Mtakatifu.
Amina
❖ Wimbo wa Roho Mtakatifu (Sekwensia)
❖ Baba yetu…….
❖ Salamu Maria….
❖ Atukuzwe Baba…
2. TAFAKARI
SIKU YA KWANZA
MADA: WEMA WA MUNGU
ANDIKO REJEA: Warumi 8:28:32
Mathayo
7:7-11
SIKU YA PILI
MADA: MCHUNGAJI MWEMA
ANDIKO REJEA: Zaburi 23
Yohana
10:11-14
SIKU YA TATU
MADA: MUNGU KAMA BABA
ANDIKO REJEA: Mathayo 6:26-34
SIKU YA NNE
MADA: BIDII KATIKA KAZI
ANDIKO REJEA: Mithali 22:29
1
Wathesalonike 4:11-12
SIKU YA TANO
MADA: USAFI WA MOYO
ANDIKO REJEA: 1 Petro 2:11- 12
Tito
2:111-15
SIKU YA SITA
MADA: ELIMU
ANDIKO REJEA: Mithali 4:10- 13
2
Timotheo 3:16
SIKU YA SABA
MADA: NALIMTUMAINIA MUNGU
ANDIKO REJEA: Isaya 41:10
Luka
12:7
SIKU YA NANE
MADA: SALA
ANDIKO REJEA: Mathayo 6:5 -15
SIKU YA TISA
MADA: SHUKURANI
ANDIKO REJEA: Luka 17: 11-19
3. NOVENA KWA
MTAKATIFU YOSEFU MFANYAKAZI
NIA ZA NOVENA
- Tunawaombea mapadre wetu wapya Katika Parokia yetu ili waweze kutenda utume wao kwa weledi mkubwa wakisaidiwa na msaada wa neema ya Mungu.
- Tunawaombea wanajumuiya wapya wa mwaka wa kwanza Mungu awape neema ya kudumu Katika maisha ya sala na jumuiya bila kurudi nyuma .
- Tunaombea muhula wetu mpya wa masomo ukawe heri kwa wanajumuiya wote. Roho mtakatifu akatuongoze tukapate kufanya vyema Katika masomo yetu na afungue njia zetu tuweze kutimiza malengo yetu.
- Tunaomba umoja katika jumuiya yetu, wanajumuiya wote tukawe na umoja na ushirikiano katika safari ya maisha yetu.
- Tunawaombea viongozi wote wa jumuiya katoliki Muhimbili nguvu ya Mungu Katika kutimiza utume wao.
SIKU
YA KWANZA
Baba Yosefu, ulimfundisha Yesu jinsi ya kusali, kucheza na
kufanya kazi, utusaidie kutambua kwamba tunaweza kupata elimu kwa kusikiliza na
kujifunza. Tukiwa na wewe ambaye unatusaidia na kutuongoza, tunaomba, ee Mt.
Yosefu, utuombee tuchague njia sahihi na tubaki kuwa waaminifu katika
mafundisho ya Yesu. Amina.
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA PILI
Mt. Yosefu, ulimwokoa na kumhudumia Neno wa Mungu, na chakula
cha uzima kilichoshuka kutoka mbinguni. Uwaangalie mapadri wa Kanisa, ambao
asili yao ni nyumba uliyoiongoza, na uwaombee ili nao pia, waweze kuwahudumia
kwa uvumilivu watu waliowekwa chini ya uangalizi wao. Tunaomba mapadri
wawafundishe kiaminifu waamini Neno la Mungu na kuumega mkate, wa uzima kila
siku, kwa ajili yao.Tunaomba wawaimarishe katika imani na matumaini,
wakiwafariji katika magumu na katika nyakati za kukukatisha tamaa. Pia umuombe Yesu
wetu awavishe taji kwa kazi zao na utumishi wao kwake hapa duniani kwa
kuwashirikisha uzima wa milele pamoja nawe Mbingguni milele na milele.
Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba
Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU
YA TATU
Mt. Yosefu Mwenyeheri, sala zako zinaweza kufanya mambo
yasiyowezekana, yakawezekana. Tunakuomba uje kutusaidia katika shida na magumu
tuliyonayo sasa. Uweke kwenye ulinzi wako shida na mahangaiko yetu tunayoyaleta
kwako na utuombee, ili tuweze kupata msaada kadiri ya mapenzi ya Mungu. Baba
yetu mpendwa, tunakutegemea kabisa, na kwa imani, tunajikabidhi kwako kama
watoto wadogo waliyolala mikononi mwa baba zao. Isisemekane kamwe, kwamba
tumekuomba bila mafanikio. Yesu na Maria hawawezi kukukatalia chochote
unachowaomba. Kwa matumaini hayo, tunakuomba udhihirishe wema na Upendo wako
mkubwa kama ilivyo nafasi yako kwa mchumba wako, Bikira Maria, na Mwanao Yesu.
Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA NNE
Mpendwa Mt. Yosefu,
wewe ni msimamizi wa familia ya kanisa. Mungu alikuteua uwe kiongozi na mlinzi
wa Familia Takatifu ya Nazareti. Ulichagua kufanya kazi ya useremala, amabayo
iliwafanya baadhi ya watu waulizane juu ya Yesu wakisema; “Huyu amepata wapi
hekima hii na miujiza hii? Huyu si mwana wa seremala?” Tunaomba kwa sala zako,
uwabariki na kuwatia moyo mafundi seremala wote ambao kazi zao ni sawa na ya
kwako. Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA TANO
Mt. Yosefu,
Mwenyeheri, mume wa Bikira Maria, uwe nasi katika siku hii ya leo. Ulimlinda na
kumthamini Bikira Maria. Ukimpenda mtoto Yesu kama mwanao wa kumzaa, ulimwokoa
kutoka katika hatari ya kifo. Ulilinde Kanisa, nyumba ya Mungu, lililokombolewa
kwa damu ya Yesu. Mlinzi wa familia Takatifu, uwe nasi katika majaribu.
Tunaomba utuombee tujaliwe nguvu ya kuziepuka dhambi na kuzishinda nguvu za
dhambi ili katika maisha tuweze kukua katika utakatifu na baada ya kufa,
tuvikwe taji la ushindi na kufurahia milele na milele. Amina.
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA SITA
Ee Mt. Yosefu, ambaye ulinzi wako ni mkubwa, wenye nguvu na
wa haraka mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, tunakukabidhi mahitaji na haja za
mioyo yetu. Ee Mt. Yosefu utusaidie kwa maombezi yako yenye nguvu na utuombee
kwa Mungu atupatie Baraka zote za kiroho kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
ili kwa nafasi yako Mbinguni tuweze kumsifu na kumheshimu Baba Yetu wa milele.
Ee Mt. Yosefu, kamwe hatutachoka kukufikiria wewe ukiwa umembeba Yesu, akiwa
amelala mikononi mwako. Hatuthubutu kumsogelea akiwa amepumzika hivyo karibu na
moyo wako. Tunakuomba umguse kwa kwa niaba yetu, umbusu, umuombe nae atubusu
wakati tutakapovuta pumzi yetu ya mwisho. Mt. Yosefu, msimamizi wa wanakufaa,
utuombee. Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA SABA
Ee Mt.Yosefu, mfano wa wote wanojituma kufanya kazi, utujalie
neema ya kufanya kazi kwa moyo wa toba kwa malipizi ya dhambi zetu nyingi;
kufanya kazi kwa bidii kwa kuweka mbele upendo wa kufanya kazi; kuliko vionjo
vyetu; kwa shukrani na furaha, kuona ni heshima kutumia na kukuza zawadi
tulizopewa na Mungu, kwa njia ya kufanya kazi kwa utaratibu, amani na kwa kiasi
na uvumilivu, pasipo kulegea kwa uchovu, au ugumu wa kazi; zaidi ya yote, kwa
nia njema kabisa na kujikana wenyewe, tukikumbuka daima kifo na maelezo
tunayotakiwa kuyatoa kwa muda tuliopoteza, talanta tulizofukia, mema ambayo
hatujayatenda na kujiona sana katika mafanikio, kitu ambacho ni hatari katika
kazi ya Mungu. Yote kwa Yesu, Yote kwa Maria, yote kufuata mfano wako, ee Baba
wa imani Mt. Yosefu! Hii itakuwa ndio kaulimbiu yetu maishani mwetu na milele.
Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA NANE
Ee Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko
yetu; na kisha omba shime ya Mchumba wako mtakatifu tunaomba pia kwa matumaini
usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira mtakatifu mzazi wa
Mungu, na kwa ajili ya kumtunza mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie kwa wema
siye tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tukakombolewa kwa damu yake. Tusimamie
katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako. Ee mlinzi amini wa jamaa
takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristo. Ee baba uliyetupenda mno
tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji,
utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao
gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na
leo hivi likinge kanisa takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika
shida yote, Mtunze daima kila mmoja wetu kwa mfano wako, ili tupate msaada
wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya
raha milele. Amina
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SIKU YA TISA
Mt. Yosefu, ututazame, sisi tuliyekuchagua wewe leo hii uwe
msimamizi watu wakati wa uhai wetu na katika saa ya kufa kwetu. Ututazame na
kutuzidishia moyo wa sala na wa kumtumikia Mungu. Ufukuze mbali nasi kila aina
ya dhambi, utuombee ili kifo kisitujie tukiwa hatujajiandaa, bali tupate muda
wa kutubu dhambi zetu zote kwa njia ya sakramenti ya kitubio katika hali ya
majuto kamili, ili saa ile ya kufa kwetu tukabidhi roho zetu mikononi mwa Yesu
na Maria. Amina.
Ee Mt. Yosefu Mfanyakazi, leo tunakuja mbele yako, tukiomba
kwa maombezi yako tujaliwe (………...Hapa
taja Ombi lako)
Baba Yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe Baba x 3
SALA YA MWISHO
Ee bwana wetu Yesu kristo, tunaleta maombi yetu maalum kwako ingawa hayatimizi kamwe kwa ukamilifu mahitaji yetu na matamanio mengi yaliyomo moyoni mwetu. hatuombi kutimiziwa tu maombi yetu hayo bali Neema ya kukutegemea wewe katika kutimiza kiu ya mahitaji na matamaniao ya mioyo yetu ulivyotupatia wewe. Tunakuomba Bwana Yesu ujibu sala na maombi ya waja wako walioungana nasi katika kusali Novena hii. Tunakuomba uwabariki kwa pendo lako na uwatakatifuze. Tunakuomba kwa mioyo yetu iliyo wazi kabisa tukijua kuwa haitatufaidia chochote tukivipata vya ulimwengu huu na kuipoteza nafsi zetu. Ee bwana Yesu Kristu, tusaidie daima kuona wema na utukufu wako katika majaribu yetu yote. Tusaidie pia kuona Baraka zako kila siku na daima kukupenda zaidi na zaidi. Asante bwana Yesu kwa kila kitu kwetu. Amina
4. KUFUNGA
Sala ya kuomba kifo chema
Ee Yesu na
Maria na Yosefu, nawatolea moyo na roho na uzima wangu,
Ee Yesu na
Maria na Yosefu, mnijie saa ya kuzimia roho yangu,
Ee Yesu na Maria na Yosefu, mnijalie nife mikononi mwenu.
Tunaukimbilia
Tunaukimbilia ulinzi wako, Mzazi Mzazi Mtakatifu wa Mungu. Usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, Ee Bikira Mtukufu na mwenye Baraka. Amina
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. AMINA

إرسال تعليق